MFUMO wa stakabadhi ghala umetajwa kuboresha masoko ya mazao kwa wakulima na kuwafanya kupata tija na kutambuliwa na taasisi za kifedha zinawawezesha kupata mikopo mbalimbali.
Mfumo huo umeweza kuwasaidia wakulima kutolanguliwa mazao yao na watu wa kati ‘madalali wa mazao na kupelekea wakulima kupata tija ya mazao yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, amesema kuwa mfumo huu umeimarika “mfumo sasa umeimarika tunatekeleza kwenye mikoa 23 kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara na tuna bidhaa 18 zinazopita kwenye mfumo huu tija sasa inaonekana waziwazi”
Amesema kuwa tija hiyo inaonekana kwa wazalishaji mali yaani wakulima na kwa Halmashauri katika kukusanya tozo zao.
Amesema kuwa Mfumo unafanya ukusanyaki kupitia vyama vya ushirika, wakusanyaji wengine ni wafanyabiashara wenye leseni za kufanya biashara huko nyuma walikuwa wanatambulika kama madalali lakini sasa wananuzi hawa wananunua kwa bei ya sokoni kwa kuwa zinatolewa kwa uwazi.
Amesema kuwa mazoa hayo yakiingizwa gharamani huwekwa kwenye kazidata ya bodi ya stakabadhi ghalani, “kazidata hiyo ndio inayotumika na wenzetu wa soko la bidhaa na ukizungumza na sisi basi lazima uzungumze na pacha wetu muuzaji soko la bidhaa Tanzania, wao wanauza mazoa yao kidigitali na kusema kweli tumefaidika na tumeona umuhimu wa kutumia mfumo huu tukishirikiana na wamiliki wa mazao kama mazao yenye bodi basi tunashirikiana na bodi hizo lakini kwa yale mazao yasiyokuwa na bodi basi sisi tunashirikiana na Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko”.
“Kwa umoja wetu tunaweza kuhakikisha mkulima yule na lile zao lake alililolitolea jasho anakwenda sokoni akirejea na tija zaidi,”alisema Bangu.
Bangu amesema kuwa tayari zao la korosho kupitia mfumo huo kwa limeuzwa kiasi cha zaidi ya tani 400,000. Na Mbaazi zaidi ya tani 200,000, ufuta tani 200,000, na sasa zao la Choroko linaendelea kuuzwa ambapo kwa sasa zishauzwa tani 60,000, .
“Unaweza kuona hata yale mazoa hayakuwahi kutegemewa kama mazoa ya kibishara sasa yanakuza uchumi wa mkulima,”amesema Bangu.
Amesema sasa wakulima wamekuwa wanatambulika na taasisi za kifedha jambo ambalo linamewahahakikisha kupata mikopo, “kimsingi tumerasmisha biashara ya mazoa”.
Bangu amesema kuwa mfumo huo unatoa ajira “kwenye kila ghala ukitoa mmiliki wa ghala kunakuwa na wafanyakazi watano pale nimekuwa nikishuhudia vijana wanaomaliza vyuo vikuu na kuja kujiunga na sekta ikiongezeka,”.
Amesema kuwa mfumo huo upo kwenye mikoa hiyo 23 na kuwashauri wakulima wote kupitisha mazao yao kwenye mfumo huo .
Bangu amesema kuwa bodi hiyo inaendelea kuwekeza kwenye maghala ya ndani na kuziingiza kwenye mifumo maghala mapya ikiwa pamoja na kuhakikisha kuwa soko la ndani linaendelea kuleta tija.
Amesema kuwa jukumu la kudhibiti ubora wa bidhaa na mazao bodi hiyo imelikabidhi kwa msimamizi wa ghala ambaye anajukumu la kuhakikisha kuwa hakuna bidhaa au zao litakaloingia likiwa halina ubora naye atahakikisha mnunuzi naye anachukua bidhaa yenye ubora.
Amesema kuwa wakulima hawalazimishwi kuuza mazao yao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani lakini kwa yale mazao yenye bodi ni lazima mazao hayo yaratibiwe na bodi husika.
Amewakaribisha wadau mbalimbali wa kilimo na stakabadhi ghalani kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa mfumo huo ambapo kutakuwa na maonesho katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kuanzia tarehe 28 mpaka 30 Aprili mwaka huu.
Akielezea kuanzishwa kwa mfumo huo amesema kuwa ulianzishwa baada ya kubainika kuwa hiyo ndio njia itakayomaliza changamoto za soko kwa wakulima na kuhakikisha kilimo kinakuwa kina tija.
“Kimsingi mfumo huu ulianza kufanyiwa utafiti tangu 2000 ulipoonekana unaweza kuwasaidia wakulima na wazalishaji mbali maana ulionekana unaweza kufanya kazi kwa wakulima na pia kwa wazalishaji wengine ambao sio wakulima.
“Katika kuliona jambo hili na faida yake basi mwaka 2006 ikanzisha bodi ambapo sheria ilitungwa 2005 na kanuni ziliaanza 2006 na taasisi ikaanza kipindi hicho hicho kuanzia hapo mfumo ukaanza katika hatua tofauti tofauti kama mtoto kuna nyakati za kutembea, kusimama na kukimbia anavyokuwa na niwashukuuru Watanzania kwa kuendelea kuonesha nia ya kuutumia mfumo huo.
Kwa upande wake David Sukali, Mkuu wa kitengo cha Manunuzi bodi ya usimamazi wa Stakabadhi za ghala, amesema kupitia mfumo huo umewawezesha wakulima kupata mikopo na nafuu zote za kifedha.
Akizungumzia manufaa ya mfumo huo Sukali amesema kuwa “Mfumo huu unamanufaa makubwa unapotumika hususani katika mazao tukiinza na zao la korosho mathalan kwenye bei na wanunuzi kupata uhakika wa mazao,
Mbali na hilo amesema kuwa mfumo huo umewezesha wakulima kuwa karibu na soko na hivyo kurahisha kuuza mazoa kwa bei yenye tija na kwa haraka,
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi ghala (WRRB) Asangye Bangu



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...