Shule ya Brookside Academy ya Jijini Dar es Salaam imewataka wazazi kupeleka watoto shuleni hapo ili wapate elimu bora , shule hiyo ni ya Mtaala wa Kiingereza.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa maonyesho ya Shule hiyo Mlimani City Jijini Dare es Salaam, Mwalimu Gloria Hamis alisema kuwa mbali na elimu bora pia shule hilo inafundisha masomo ya lugha za Kimataifa zikiwamo Kifaransa na Kichina.
“Naomba Wazazi walete wanafunzi wao Shuleni kwetu kwa lengo la kupata elimu bora na mazingira mazuri ya kujifunzia ,”
Shule hiyo iko Kimara Suka, Wilaya ya Ubungo Pia imekuwa ikifanya vizuri kimasomo kila mwaka kwenye mitihani ya kimataifa, mara kadhaa imekuwa Kinara wa matokeo ya Darasa la Saba Wilaya ya Ubungo.
Wataalamu wa elimu wanasema shule hiyo ni model School kwani inafata taratibu bora za kielimu na Kiutawala na yenye mifumo imara ya kujiendesha.
Usafiri ni wa kuaminika kwa wanafunzi na chakula bora kwa watoto kinachozingatia misingi ya ukuaji wao, anafafanua Mwalimu Gloria.
Shule ni mchanyiko Wavulana na Wasichana , inafundisha masomo ya awali na Elimu ya Msingi.
Wazazi wanakaribishwa kutembelea banda la shule hiyo kwenye maonyesho yajayo wakati wa sikukuu za Pasaka tarehe 5 na 6 mwezi April na Kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba tarehe 28 June hadi 13 Julai mwaka huu.
Mawasiliano yao ya simu ni 0742 100 790
Muonekano wa banda la Shule hiyo.
+



.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...