Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imeendelea kudhihirisha ubora wake katika utoaji wa huduma baada ya kushika nafasi ya pili kwa miaka miwili mfululizo, miongoni mwa mamlaka 20 za maji nchini zenye wateja zaidi ya 20,000, tuzo hizo hutolewa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA).
Mafanikio hayo yametokana na tathmini ya utendaji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 inayofanywa na EWURA, ambayo hupima mamlaka za maji kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo ubora wa huduma kwa wateja, ukusanyaji wa mapato, upatikanaji wa maji safi na salama, pamoja na usimamizi wa miundombinu ya maji na majitaka.
Ripoti hiyo imezinduliwa rasmi na Waziri wa Maji, Jumaa H. Aweso, Machi 19, 2026, Mjini Morogoro, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha uwajibikaji na ufanisi katika sekta ya maji.
Ufanisi huu unatokana na mshikamano wa Bodi ya Wakurugenzi, watumishi wa mamlaka, pamoja na ushirikiano wa wananchi, sambamba na uwekezaji unaoendelea katika kuboresha huduma za maji katika Manispaa ya Songea.
Mafanikio haya yanaonyesha kuwa juhudi za pamoja na usimamizi thabiti vina mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha huduma za maji, na yanaweka msingi imara wa kuendelea kuboresha zaidi huduma kwa wananchi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...