Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imejipanga kuhakikisha matumizi ya Nishati Safi ya kupikia  kupitia mradi wa Rafiki Briquete yanaongezeka katika mikoa mbalimbali nchini ili kufikia asilimia 86 ya matumizi ya  Nishati Safi ifikapo mwaka 2030.


Hayo yameelezwa leo Machi 12, 2026 Mkoani Tabora na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya  Bunge ya Nishati na Madini ilipokuwa ikikagua miradi inayosimamiwa na Wizara ya Madini.

Dkt. Kiruswa amesema kuwa, STAMICO  tayari imeshanunua Mitambo minne yenye uwezo wa  kuzalisha tani 20 kwa saa ambayo imesimikwa katika  maeneo  ya Kiwira,  Pwani, Chigongwe Mkoani Dodoma na   Kiloleni Mkoani Tabora.

Dkt. Kiruswa amefafanua kuwa, kwa Mkoa wa Tabora, STAMICO imelenga kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi kwa  wakulima wa Tumbaku ambao kwa muda mrefu  wamekuwa wakitumia kuni kwa wingi suala linalohusisha uharibifu  wa mazingira. 

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Subira Mgalu  ameipongeza STAMICO kwa ubunifu wa miradi endelevu  yakimkakati  inayoleta mchango mkubwa kwa taifa ikiwa pamoja na  kuunganisha mnyororo mzima wa thamani madini.

Mgalu ameitaka STAMICO kuanza uzalishaji mapema  pamoja na  kufungua matawi mengine katika mikoa mbalimbali nchini ili kutekeleza Agenda ya kitaifa inayohusu  matumizi ya Nishati Safi ili kufikia  asilimia 86 za matumizi ya Nishati Safi ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake  Msafiri Mbibo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini , ameishukuru kamati kwa maoni mbalimbali yaliyolenga uboreshaji wa mradi huo hususan katika upande wa ajira na  Usimikaji wa mitambo ya Uzalishaji.

Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo  Deusdedith  Magala, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa STAMICO, amesema kuwa mradi wa Rafiki Briquettes katika Mikoa mbalimbali unatarajia kuajili watanzania zaidi ya 100




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...