Na Farida Mangube, Morogoro
Wanawake wametakiwa kutumia kikamilifu fursa za masomo na mafunzo zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kujijengea uwezo, kuongeza ujuzi, na kuimarisha ushiriki wao katika maendeleo ya jamii.
Wito huo umetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Amandus Muhairwa, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanawake wa chuo hicho katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Prof. Muhairwa amesema kuwa chuo kina mfumo thabiti wa kulinda wanawake na wasichana pamoja na kutekeleza mpango mkakati wa usawa wa kijinsia, hali inayochangia kuwepo kwa mazingira salama, yenye utulivu na yanayowezesha wanawake kufikia malengo yao ya kitaaluma na kiutendaji.
Kwa upande wao, Mwenyekiti wa RAAWU tawi la SUA, Bw. Faraja Kamendu, na Mwenyekiti wa THTU tawi la SUA, Bw. Nickson Mkilamwene, wamesema kuwa kuwapa wanawake nafasi katika ajira na uongozi kunachochea ufanisi wa utendaji kazi katika taasisi mbalimbali.
Viongozi hao pia wamewahamasisha wanawake kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya chuo na kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kulinda maslahi yao ya kikazi na kitaaluma.
Akisoma hotuba kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wanawake wa chuo hicho, Bi. Farida Mkongwe ameishukuru menejimenti ya chuo kwa kuendelea kutoa fursa za mafunzo kwa wanawake, akisema hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ujuzi, uwezo na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi.
Ameongeza kuwa utoaji wa mafunzo kwa watumishi unazingatia mipango na bajeti ya chuo, huku akiiomba menejimenti kuendelea kupanua wigo wa fursa hizo ili kuwajengea wanawake uwezo zaidi katika nyanja mbalimbali za kitaaluma na kiutendaji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, amesema mkoa huo umeendelea kuwa kinara katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kama sehemu ya kutambua mchango wao muhimu katika maendeleo ya jamii.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Shule ya Msingi Fulwe, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Malima amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali kuvumilia vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake, hususan wanapopoteza wenza wao.
Amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya vitendo hivyo ili kulinda haki, usalama na ustawi wa wanawake katika jamii.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...