Taasisi ya Ramadhan Charity Programme 2026 imewataka Watanzania kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa wamoja, kusaidiana na kufanya kazi kwa pamoja katika kuwasaidia watu wenye uhitaji katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Ramadhan Charity Programme 2026, Ahmed Misanga, wakati akikabidhi sadaka ya iftar katika kituo cha Jaamiul-Furouq, kilichopo wilayani Manyoni mkoani Singida.

Misanga amesema kuwa kutoa sadaka kunahitaji moyo wa kusaidia na si lazima mtu awe tajiri. Ameongeza kuwa watu wenye uwezo wajitokeze kushirikiana katika kuwasaidia wenye uhitaji, kwani wapo wengi hasa katika vituo vya kulea watoto yatima na watu wasiojiweza.

Aidha, Misanga amesisitiza kuwa kutoa sadaka na kutumia mali katika njia ya Allah ni miongoni mwa matendo mema na bora, kwani hufuta madhambi na makosa kama vile maji yanavyozima moto.

Katika hatua nyingine, amewahimiza vijana kusoma kwa bidii ili wawe watu wema katika jamii na baadaye waweze kusaidia wengine wenye uhitaji.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa kituo hicho Nawawi Salimu, ameishukuru Taasisi ya Ramadhan Charity Programme 2026 kwa kuendelea kutoa sadaka ya iftar katika kituo hicho kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Amesema msaada huo umekuwa na mchango mkubwa kwa wanafunzi wa kituo hicho, na amewahimiza wadau hao kuendelea na moyo huo wa kusaidia jamii, bila kuishia katika kituo hicho pekee bali kufikia pia vituo vingine vyenye uhitaji.

“Mimi pamoja na wanafunzi wangu hatuna cha kuwalipa, lakini tunaamini Mwenyezi Mungu ndiye atakayewalipa kwa wema huu mlioufanya,” amesema Nawawi.

Aidha, amewaomba wadau wengine kuiga mfano wa Ramadhan Charity Programme 2026 kwa kuwafikia walengwa na kutoa sadaka katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwani bado kuna uhitaji mkubwa.

Ameongeza kuwa katika kituo hicho kuna zaidi ya watoto 100 wanaopata elimu ya dini na malezi ya mazingira, huku akisema milango ya msaada bado ipo wazi kwa yeyote mwenye nia ya kusaidia.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...