Na Said Mwishehe,Michuzi TV
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) imesema imeendesha kesi 1,016 zikiwamo kesi mpya 755 zilizofunguliwa mwaka 2024/25 katika ngazi mbalimbali za Mahakama nchini.
Akizungumza leo Machi 30,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Raos Dk.Samia Suluhu Hassan ,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Chrispin Chalamila wakati akikabidhi taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo 2024/2025 amesema katı ya kesi hizo mpya, 10 zimefunguliwa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Amesema pia kesi 593 zimetolewa uamuzi Mahakamani,ambapo Jamhuri imeshinda kesi 483. Hilo ni ongezeko ikilinganishwa na kesi 440 zilizotolewa uamuzi na kesi 334 zilizoshinda mwaka 2023/2024.
Amesema kuwa kwa mwaka 2024/25, kiwango cha kushinda kesi ni asilimia 81.5. Kiwango hiki kimeongezeka I kilinganishwa na kiwango cha asilimia 76 kilichofikiwa mwaka 2023/24.
Wakati huo huo amesema kazi nyingine zilizofanyika ni uchunguzi wa majalada 169 yanayohusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha ya mapato katika Halmashauri mbalimbali.
Amefafanua uchunguzi ulibaini Sh.bilioni 12.3 kilikusanywa kwa mashine za kukusanyiaushuru (POS) kupitia mfumo wa kielektroniki wa kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya ndani pasipo kuwasilishwa benki.
“Kati ya majalada yaliyochunguzwa: majalada 32 yanaendelea na uchunguzi; majalada 39 yamewasilishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuomba kibali cha mashtaka na majalada mawiliyalipata kibali cha kufunguliwa mashtaka Mahakamani;
“Majalada 49 kesi zinaendelea Mahakamani; majalada nane watuhumiwa wamechukuliwa hatua za kinidhamu; na majalada 39 yalifungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.Kupitia uchunguzi huu, TAKUKURU ilioko fedha Sh.bilioni moja na tunaendelea na uchunguzi ili kuhakikisha kuwa kiasi chote kilichofanyiwa ubadhirifu kinarejeshwa.”
Aidha amesema kupitia operesheni walizofanya uchunguzi wa TAKUKURU sababu za ubadhirifu kuendelea kufanyika kwenye ukusanyaji wa mapato ya halmashauri mbalimbali nchini ni pamoja na sababu kuu mbili.
Ametaja sababu hizo ni kukosekana kwa usimamizi madhubuti wa kuhakikisha kuwa fedha inayokusanywa inahifadhiwa benki pamoja na baadhi ya wasimamizi na wahasibu kukosa uadilifu na kujinufaisha na fedha hiyo.
“Kazi nyingine iliyofanyika ni uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh.milioni 861.2 za Chama cha Msingi cha KISANGA Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, ambapo ubadhirifu huo umefanywa na viongozi wa chama hicho wakishirikiana na maafisa ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge. Uchunguzi wa jalada hili umekamilika na watuhumiwa wamefunguliwa kesi Mahakamani.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...