Na WAF-Korogwe

Mganga Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt. Japhet Simeyo amesema kikao kazi cha tathmini ya matukio na athari za kiafya kitawajengea uwezo wataalam kwenye mkoa huo ili wawe tayari kuzuia na kukabiliana na majanga yatokanayo na dharura.

Dkt. Simeyo ameyasema hayo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga leo Machi 02, 2026 katika kikao kazi cha tathmini ya matukio na athari za kiafya katika mkoa wa Tanga, kilichoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya PATH& CIHEB.

"Mkoa wa Tanga umekuwa na Majanga mbalimbali yanayotokea ikiwa ni pamoja na moto, ajali za barabarani, Magonjwa ya Milipuko na mabadiliko ya Tabianchi" amesema Dkt.Simeyo na kuongeza

"Mafunzo haya yamekuja kwa wakati muafaka kwani yatawajengea uwezo baina ya sekta mtambuka kwa kupitia za majanga yaliyowahi kutokea na kuimarisha afua za udhibiti wa majanga hayo kabla hayajatokea"  amesema Dkt Simeyo

Kwa upande wake Mratibu-Udhibiti Athari za Majanga Wizara ya Afya, Dkt Saumu Nungu amesema kuwa kikao kazi hicho kinalenga kuainisha athari ambazo zinaweza kusababisha majanga na dharura katika mkoa wa Tanga na kuandaa mpango kazi ambao utasaidia mkoa kujiandaa vizuri.

"Pamoja na hilo kikao kupitia kikao hiki tutandaa kalenda itakayokuwa inaonyesha wakati ambao majanga yanaweza kutokea yaani Tanga Region Health Profile Risk and Calendar" amesema Dkt Saumu

Amefafanua kuwa kupitia kalenda ya matukio, timu za kukaliana na majanga ya dharura zitaweza kujiandaa mapema kabla ya kipindi ambacho athari hizo zina uwezekano wa kutokea, hivyo kuleta tija na kulinda afya za wananchi dhidi ya athari za majanga hayo.

Naye Dkt. Said Sheuya kutoka PATH&CIHEB amesema kuwa, Taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na mapambano ya magonjwa ya mlipuko na ufuatiliaji wa magonjwa, ushirikiano wa mfumo wa Afya Moja, kuhakikisha uwepo wa mifumo ya afya inayosomana katika utoaji wa taarifa za magonjwa, na kufanya mafunzo kwa timu za kupambana na dharura katika mikoa.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...