*Zimo dawa aina ya Pethidine, Morphine na Fentanyl ni dawa tiba zenye asili ya kulevya

*Basi linalofanya safari Tanzania ,Uganda ,Congo lahusishwa,pia Scania lenye namba za Afrika Kusini 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata tani 9.93 za dawa za kulevya aina mbalimbali, chupa 1,795 za dawa tiba zenye asili ya kulevya na kuteketeza ekari 87.5 za mashamba ya bangi. 

Aidha imekamata Magari 6 na pikipiki 29 vilikamatwa katika operesheni
hizo huku watuhumiwa 151 wakikamatwa kuhusika na uhalifu huo.
Aidha, kwa kushirikiana na maafisa wa kituo cha forodha cha Mutukula, 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine boksi 105 zenye chupa 1,045, Morphine Sulphate boksi 31 zenye chupa 310 na Fentanyl boksi 44 zenye chupa 440.

Akizungumza leo Machi 4,2026 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana a Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema dawa hizo zilikamatwa katika basi la abiria la kampuni ya SR Classic lenye usajili wa nchi ya Congo namba 5673AB04.

Amesema basi hilo linalofanya safari zake kati ya nchi za Uganda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Dawa zilizokamatwa zilibainika wakati wa upekuzi wa basi hilo katika kituo cha forodha cha Mutukula lilipokuwa likiingia chini Tanzania.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika tukio hilo ni Hassan Omary Mwambashi maarufu kama Macheni (50) mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Ibrahim Saidi Malindi (36), manzania anayeishi Kampala Uganda, Yassa Said Hamood (38) mkazi wa Magomeni Dar es Salaam.

Wengine ni Hamad Said Hamad (46) mkazi wa Mombo Tanga, Abdul Athuman Khamis (31) mkazi wa Amana, Dar es Salaam, Mohamed Abdallah Sako (34) mkazi wa llala, Mwinshaa Mohamed Abdalla (47) mkazi wa Magomeni Dar es Salaam.

“Dawa aina ya Pethidine, Morphine na Fentanyl ni dawa tiba zenye asili ya kulevya zilizopo kwenye kundi la afyuni (opioids) ambazo hutumika hospitalini kwa ajili ya kupunguza maumivu makali wakati wa operesheni, kwa wagonjwa wa saratani, ajali, pamoja na wagonjwa wa selimundu.

“Aidha, dawa hizi zikichepushwa zinaweza kutumika kama dawa za kulevya na kusababisha uraibu kwa haraka zaidi kutokana na kuwa na nguvu kubwa. Dawa hizi zipo katika kundi la vipumbazi na zinauwezo mubwa wa kusababisha vifo kwa haraka kwa mtumiaji kwani huharibu mifumo ya mwili hasa mapigo
ya moyo, mfumo wa fahamu na fumo wa upumuaji.

“Hapa chini, dawa zilizokamatwa zinadhibitiwa kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Sura ya 95 na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba ya TMDA Sura ya 219. 

“Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeorodhesha dawa hizo katika Jedwali la Kwanza (First Schedule) na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba inabainisha kuwa, muingizaji na msambazaji wa dawa aina ya nakotiki ni Medical Store Department (MSD) pekee.”

Kwa upande wa dawa za kulevya, bangi aina ya skanka Kamishina Jenerali Lyimo amesema Mamlaka imeendelea kukamatwa kwa wingi nchini. Katika operesheni zilizofanyika Dar es Salaam, muhumiwa Jontwa Samwel Mwaikonyole (43) mkazi wa Gogoni Kibamba, alikamatwa kiwa na kilogramu 81.883 za skanka.

Amefafanua dawa hizo zilikutwa ndani ya gari aina ya Scania lenye namba za usajili wa chi ya Afrika ya Kusini CAA 129054 na trailer namba CAA 22911 lililokuwa limebeba matunda aina ya apples.

Aidha amesema katika eneo la Chanika Buyuni watuhumiwa Masudi Rajabu (38) na mwenzake Shafii Mohamed (30) walikamatwa wakiwa na kilogramu 488.64 za skanka.

Aidha, katika ukaguzi wa mabasi ya abiria jijini Mbeya, watuhumiwa sita walikamatwa kwa nyakati tofauti wakisafirisha bangi aina ya skanka. Watuhumia hao ni Lenard Paulo (21) mkazi wa Sirali Mara, alikamatwa na kilogramu 46.46, Maria Kandonga (18) na wenzake Monica Kandonga (41) na Ibrahim Mwakibete (26) wote wakazi wa Mbeya.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na kilogramu 9.68, mtuhumiwa Joseph Mkwala (30) raia wa Malawi alikamatwa na kilogramu 4.62 na Esther Mbise (22) mkazi wa Mbeya alikamatwa na kilogramu 16.1 za skanka.

Wakati huo huo mkoani Arusha, watuhumiwa Fatuma Mussa Mohamed (45) maarufu kwa jina la Mama Arapha na mwenzake Elibaraka Martin Kingu (29) maarufu kwa jina Baraka walikamatwa wakiwa na bunda 937 za mirungi zenye uzito wa kilogramu 363.45. 

“Mama Arapha ni mhalifu wa muda mrefu aliyekuwa akiendesha mitandao ya safirishaji wa mirungi.”

Katika hatua nyingine amesema katika operesheni zilizofanyika mikoa ya Tabora, Tanga, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Katavi, Mtwara, Mara, Morogoro, Kigoma, Ruvuma na Kilimanjaro zilikamatwa tani 5.24 za dawa za kulevya aina ya bangi, tani 4.04 za mirungi pamoia na gramu 72 za heroin.

Hata hivyo katika operesheni zilizofanywa na mamlaka hiyo pia wamefanikiwa kukamata magari sita 6 na pikipiki 29 vilikamatwa katika operesheni hizo huku watuhumiwa 151 wakikamatwa kuhusika na uhalifu huo.

Amesema operesheni zilizofanyika zinaonesha jitihada za Serikali katika kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya chini. Mamlaka itaendelea kupambana na wafanyabiashara haramu wa dawa za kulevya pamoja na dawa tiba zenye asili ya kulevya ili khakikisha hazichepushwi na zinawafikia wagonjwa wanaohitaji dawa hizo badala ya kutumiwa na wahalifu kama mbadala wa dawa za kulevya.

“Mamlaka itaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za Serikali, Mashirika, Asasi za kiraia pamoja na makundi mbalimbai ya kijamil kuhakikisha kwamba, tatizo la dawa za kulevya linadhibitiwa kikamilifu kwani mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wetu.”










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...