Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imekamata bidhaa mbalimbali za magendo katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo viroba 50 vya mchele, madumu 10 ya mafuta ya kula na sabuni box 25 aina ya Malaika.
Kwa mujibu wa Meneja Msaidizi wa Forodha mkoa wa Pwani Bi. Melinda Matinyi bidhaa hizo za magendo zimekamatwa Machi 19.2026 kufuatia operesheni ya udhibiti wa bidhaa zinazoingizwa nchini au kusafirishwa bila kufuata taratibu za kisheria za forodha.
Amesema idhaa zilizokamatwa zimehifadhiwa katika yadi ya TRA Bagamoyo kwa ajili ya kuendelea na taratibu za kiforodha na hatua nyingine za kisheria.
Mamlaka ya Mapato Tanzania imeendelea kutoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kufuata sheria na taratibu za kodi na forodha ili kuepuka hasara na adhabu zinazoweza kujitokeza pindi wanapojihusisha na vitendohivyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...