Na Mwandishi Wetu

Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo  na Mitaji (UN CDF) limesema kuwa linaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2030 kwa kusapoti matumizi ya nishati hiyo mashuleni na katika taasisi mbalimbali za umma hapa nchini.

Akiongea wakati wa kukabidhi majiko ya nishati safi ya kisasa  katika shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaamz Peter Malika, Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa UNCDF, amesema kupitia CookFund jumla ya shilingi bilioni 26 zimetolewa kama mikopo kwa biashara ndogo na za kati (SMEs) 102 zinazojihusisha na biashara ya nishati safi ya kupikia katika wilaya 14 za Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma na Mwanza.

Bw.Malika amesema pia kuwa wanafunzi 62,000 katika shule mbalimbali nchini Tanzania wamenufaika na mpango huo, huku UNCDF ikilenga kufikia taasisi 147 za umma ifikapo Septemba mwaka huu.

" Malengo yetu ni kuunga mkono ajenda ya nishati safi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha asilimia zaidi ya 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi hapa nchini,"

" Tukiwa kama wadau, tunachukua hatua mbalimbali, ikiwemo kusaidia upatikanaji wa miundombinu katika shule mbalimbali hapa nchini na kuwa na program mbalimbali na wadau katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi ikiwemo sera za kuvutiwa wawekezaji katika sekta hii," amesema.

Ameongeza  kuwa UNCDF  wataendelea kutoa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali katika kuhakikisha nishati safi inafikiwa.

Amesema nishati safi ya kupikia inalinda mazingira na afya pamoja na kuokoa gharama inayotokana madhara ya matumizi ya mkaa na kuni.


Akiongea wakati wa kupokea msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Bunge Leonida Mlekule ameishukuru UNCDF kwa msaada huo wa kuhamaisha matumizi ya nishati safi na kuunba mkono mpango wa matumizi ya nishati safi hapa nchini.

Amesema kuwa majiko waliyoyapata kutoka UNCDF watayatunza ili kuendelea kupunguza gharama ya manunuzi.

Amesema matumizi ya mkaka yalikuwa yanaigharimu shule hiyo  zaidi ya milioni mbili, lakini kutokana na majiko hayo wameweza  kuokoa kiasi cha shilingi milioni moja na kuzipeleka katika matumizi mengine.

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo ya majiko ya kisasa alikuwa Naibu Waziri wa Nishati , Salome Makamba ambaye ameishukuru UNCDF kwa msaada huo na kuahidi ushirikiano zaidi katika kufanikisha ajenda hiyo ya matumizi ya nishati safi hapa  nchini.

" Tunaomba wadau wengine wajitokeze katika kusaidia mpango huu hapa nchini," amesema.

Mradi huo wa  kusambaza nishati safi ya kupikia katika Taasisi za Umma na Sekta Binafsi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).


Naibu Waziri amesema kuwa Taasisi za Umma na Sekta Binafsi zinazolisha watu zaidi ya  250 zinatakiwa kuwa na majiko ya kisasa yenye matumizi ya niashati mbadala ya kupikia katika kulinda afya na mazingira.

Amemtaja Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa ni kinara wa nishati safi ya kupikia na kutoa wito wa kujitokeza na kumuunga mkono.


Amesema utekelezaji waje unawahusu wadau wote ikiwemo Taasisi za Umma ,  Sekta Binafsi  na wadau wa maendeleo hapa nchini,.

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza wakati wa Makabidhiano ya Nishati ya Safi ya Kupikia kwa Shule ya Msingi Bunge zilitolewa na UN CDF jijini Dar es Salaam.
Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa UNCDF Peter Malika akizungumza kuhusiana na mikakati ya kusambaza nishati safi ya kupikia wakati hafla ya kukabidhi majiko ya kisasa ya kupikia katika shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Bunge Leonida Mlekule  kuhusiana na majiko yalitolewa na UNCDF kwenye shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya meza kuu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge mara baada ya kukabidhiana majiko ya kissa katika Shule hiyo .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...