Dar es Salaam, Machi 28, 2026 — Viongozi wa dini nchini wameeleza wasiwasi wao kuhusu kuendelea kwa ndoa za utotoni, wakibainisha kuwa changamoto ya uelewa mdogo wa sheria kuhusu umri sahihi wa kuolewa bado ni kubwa, hasa katika maeneo ya vijijini.
Akizungumza katika kikao cha kitaifa cha viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya kisheria ya ndoa kilichofanyika Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA, Sheikh Khamisi Mtaka, alisema pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kukomesha ndoa za utotoni, bado kuna mkanganyiko mkubwa kati ya sheria za nchi, mafundisho ya dini na mitazamo ya kijamii.
Alisema hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa juhudi za kupambana na tatizo hilo.
Sheikh Mtaka alifafanua kuwa kwa sasa hakuna sheria mahsusi inayokataza moja kwa moja ndoa za utotoni, isipokuwa Sera ya Elimu ya mwaka 2014 inayozuia wanafunzi kuolewa au kupata ujauzito wakiwa shuleni.
“Endapo kipengele hiki kitaingizwa pia katika mifumo ya kijamii na kidini bila kukinzana, kitasaidia kuhakikisha anayetarajiwa kuolewa anakuwa amekomaa kiakili,” alisema Sheikh Mtaka.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa sera na sheria zitakazoainisha bayana umri sahihi wa kuolewa kwa mtoto wa kike, hatua itakayosaidia kulinda haki zao na kuwapa fursa ya kufikia malengo yao maishani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Songea Catholic Institute of Technical Education, Padri Longino Kamuhabwa, alisema kuwa hata mafundisho ya dini yanasisitiza umuhimu wa ukomavu wa akili kabla ya mtu kuingia katika ndoa.
Akinukuu Biblia (Mwanzo 1:27), Padri Kamuhabwa alisema licha ya agizo la kuzaa na kuongezeka, ndoa inahitaji maandalizi ya kisaikolojia pamoja na uwajibikaji wa hali ya juu.
“Ndoa inajengwa juu ya msingi wa upendo na uwajibikaji, hivyo ni muhimu kuhakikisha mhusika anakuwa na uhuru wa kufanya maamuzi na ukomavu wa kutosha,” alisema.
Naye Afisa kutoka Msichana Initiative alisema tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo katika mikoa mbalimbali zimeonesha kuwa ukosefu wa elimu pamoja na mila na desturi bado vinachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa ndoa za utotoni vijijini.
Kwa upande wake, Wakili Lucy Gidamis kutoka taasisi hiyo aliongeza kuwa jamii nyingi bado zinaweka mbele maslahi ya kiuchumi badala ya ustawi na haki za mtoto wa kike.
Alisisitiza kuwa tatizo hilo linahitaji juhudi za pamoja kutoka serikalini, viongozi wa dini pamoja na wadau wa maendeleo ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...