Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wakulima na Wanufaika wa mradi wa mashamba ya Serikali ya Jenga kesho iliyobora(BBT)wapatao 300 katika Kijiji cha Mlazo kata Ndogowe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wamepatiwa Semina ya kufahamu changamoto ya Afya ya Akili,Afya ya Uzazi na namna ya kujinginga na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya Ngono.

Msomaji Lusinde na  Sharifa Athuman Isaka miongoni kwa vijana na wananchi wa Ndogowe wamesema kuwa Semina hiyo imewajengea Imani,matumaini,uvumilivu na uhakikika wa upatikanaji wa mazao kupitia shughuli zao za kilimo biashara

Wameongeza kwa kusema kuwa hapo awali walikuwa hawana uelewa kuhusu chanagamoto ya Afya ya Akili na Afya ya Uzazi ambapo wameahidi kutumia elimu waliyoipata kupitia semina hiyo kuongeza nguvu katika shughuli zao za kilimo biashara

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Mlazo  Mahawi Makasi amesema kuwa katika eneo hilo hawajawahi kupatiwa semina ya namna hiyo hivyo Serikali kupitia BBT imefanya jambo jema ambapo pia ameomba Semina hiyo iwe endelevu

Naye Afisa anayeshughulikia Masuala ya kijinsia,Jamii na Maendele kutoka BBT Neema  Urasa amesema kuwa kutokana na vijana hao kukaa shambani kwa muda mrefu kwa ajili ya shughuli ya kilimo biashara wameona ni vyema kukaa nao na kuzungumza nao masuala ya changamoto ya Afya ya Akili,masuala ya Afya ya uzazi na kujifunza na namna ya kujikinga na magongwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...