MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema Chama kinapata maendeleo kutokana na ukubwa wake, kusimamia, ahadi na imani kubwa ya wananchi kwa Chama.

Kauli ya Wasira imekuja siku chache baada ya Kiongozi kutoka katika chama kimoja Cha Upinzani na kudai CCM inabebwa na serikali.

Wasira meyasema hayo leo Machi 26, 2026 alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi za Chama Mkoa wa Geita ambalo ujenzi wake unatarajiwa kutumia sh bilioni 1.5.

“Tulipokuwa tunakuja mtu mmoja akanipa simu yake nimsikilize mkubwa mmoja wala sitaki kumtaja jina, anadai CCM ni Chama kinabebwa na serikali, sasa ningemwalika hapa aone tumejenga hapa atwambie kasma namba ngapi imeleta pesa Geta.

“Unajua ukikosa la kusema na mdomo unao unaweza kusema chochote kwani usiposema chochote mdomo utakosa kazi utakuwa unakula tu bila kusema na mdomo una kazi ya kula na kusema.








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...