Na. OWM- KAM

‎Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo amewataka wataalamu na wadau wa Ustawi wa Jamii kufanya kazi kwa weledi, uadilifu katika utendaji kazi hususani kwa watoto na wananchi wanyonge.

Ameyasema hayo Machi 24, 2026 Jijini Dodoma wakati alipofungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) huku akiwasisitiza wataalam hao kutumia teknolojia (mifumo ya Kielektroniki) katika utendaji kazi ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali.

‎Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama wa wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) Dkt. Mariana Makuu akizungumza kwenye kikao hicho alisema kongamano limelenga kuwakutanisha wanataaluma wa huduma za ustawi wa jamii, watunga sera ,wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo vinavyotoa taaluma za ustawi wa jamii ili kujadili kwa pamoja maswala ya kitaalamu kwa lengo kuu la kuboresha elimu ,sera na huduma za utawi wa nchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...