Watumishi wanawake wa Mamlaaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameungana na wanawake wengine kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2026 katika maadhimisho ya kimkoa yaliyofanyika Viwanja vya Barafu Mburahati, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ambaye aliwahimiza wanawake kuendelea kutumia fursa zilizopo kujiendeleza kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema, “Wanawake wana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii na taifa, hivyo ni muhimu waendelee kupewa na kutumia kikamilifu fursa zilizopo ili kufikia maendeleo jumuishi.”

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kuifikia Dira 2050.”

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.




Picha mbalimbali za matukio ya wafanyazi wanawake wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 08, 2026 leo katika viwanja vya Barafu Mburahati, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...