Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, ijipange ipasavyo kuhakikisha kuwa inachangia upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 ambayo imeainisha kuwa na uwiano wa Pato la Taifa wa shilingi trilioni 1 ifikapo mwaka 2050.
Mhe. Balozi Omar alisema hayo alipokutana na kuzungumza na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TRA wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka hiyo, ikiwa na mara yake ya kwanza Tangu ateuliwe na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya MUuungano wa Tanzania kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Alisema kuwa Dira iliyomaliza muda wake iliitaka Tanzania kufikisha uwiano wa Pato la Taifa wa dola za Marekani bilioni 90 hadi kufikia mwaka 2025 lakini makadirio mapya yanataka kiwango hicho kifikie dola za Marekani trilioni 1 ambazo TRA inatakiwa kujipanga ipasavyo kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kiwango cha asilimia 70 ili kutekeleza Dira hiyo ipasavyo.
Aidha, Mhe Balozi Khamis Mussa Omar, aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kuimarisha uhusiano wake na walipa kodi na kuitaka Manejimenti ya TRA kuhakikisha kuwa mchakato wa kudai kodi kwa hiari uendelee kuwa hivyo ili kuendeleza uhusiano na walipa kodu ambao wana mchango mkubwa wa kukuza Mapato.
Kuhusu udhibiti wa Walipakodi wasio waaminifu, Mhe. Balozi Omar, aliitaka TRA kuongeza jitihada za kudhibiti changamoto hiyo ikiwemo tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza bishaa nchini wakidai zinaelekezwa nje ya nchi lakini zinachepushwa na kubakizwa nchini pamoja na udanyanyifu wa mauziano ya kibiashara (Price Transfer), hatua ambayo inakwaza maendeleo ya kiuchumi.
Kwa upande wao, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Bw. Uledi Abass Mussa, walimhakikishia Mhe. Waziri wa Fedha kwamba TRA imejipanga kuchangia utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050 kwa kuongeza ufanisi wa makusanyo ya forodha na kodi za ndani.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, amehitisha ziara yake ya siku mbili ya kutembelea Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA jijini Dar es Salaam ambapo alitembelea na kujionea utendaji kazi wa Idara mbalimbali za Mamlaka hiyo pamoja na mifumo ya kidijiti inayotumika kurahisisha ulipaji kodi na taarifa kwa Walipakodi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...