Na Mwandishi wetu, Simanjiro
AFISA usafirishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Ismail Khalifan amefikishwa mahakamani kwa kosa la jinai la wizi wa shilingi 500,000 akiwa mtumishi wa umma.

Afisa usafirishaji huyo Ismail amefikishwa kwenye mahakama ya wilaya ya Simanjiro na kusomewa shitaka hilo la wizi wa shilingi 500,000 fedha ambazo ni mali ya Halmashauri hiyo.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Faustin Mushi amesoma shataka hilo Aprili mosi, 2026 mbele ya hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro Charles Uisso.

Mushi amesema Ismail anashtakiwa kwa kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258 (1), 265 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 R:E 2023.

Amesema Ismail anashitakiwa kwa kosa la wizi wa shilingi 500,000 alizopewa na mwajiri wake kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya magari ya halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema katika kesi hiyo ya jinai namba 7118/2026 mshtakiwa alipewa fedha hizo ili anunule vifaa vya magari ya kusambaza mitihani ya Taifa mwaka 2023 kwenye wilaya hiyo ila hakuvifikisha kwenye halmashauri hiyo baada ya kuvinunua.

Hata hivyo, hakimu Uisso alipomuuliza mshtakiwa huyo kama ni kweli amefanya kosa hilo amekana kutenda kosa hilo.

Mshtakiwa huyo ametimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja, barua ya utambulisho ya serikali za mitaa pamoja na kusaini bondi ya Sh1 milioni na kwa sasa yupo nje kwa dhamana.

Hakimu Uisso ameahirisha shauri hilo hadi Aprili 16, 2026 kwa ajili ya mshatakiwa huyo Ismail atasomewa hoja za awali (PH).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...