Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yao ili kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.

Mpogolo ametoa kauli hiyo leo Aprili 24, 2026, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa 20  na  matundu 45  ya vyoo  shule hapo, mradi unaotekelezwa kwa gharama ya sh. bilioni 1.8.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa iliyokuwepo kwa muda mrefu na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora zaidi.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kufikia ndoto zao,” amesema Mpogolo.

Aidha, ameeleza kuwa tangu mwaka 2007 shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya miundombinu, hali iliyosababisha wanafunzi kutumia vyumba  visivyokidhi mahitaji.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,  ambaye pia ni Ofisa Elimu ya Sekondari wa halmashauri hiyo,Dk. Mussa Ally, amesema ujenzi wa madarasa hayo utaongeza ufanisi wa utoaji elimu na kusaidia wanafunzi kupata elimu bora.

Amesema Halmashauri itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu kuhakikisha changamoto za miundombinu zinapungua na wanafunzi wanapata fursa sawa za kujifunza.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...