Na Mwandishi wetu.
SERIKALI imepongeza hatua ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kupata cheti cha viwango vya kimataifa cha ISO 21001:2018 kinachohusu mifumo ya usimamizi wa taasisi za elimu, hatua inayotarajiwa kuimarisha ubora wa mafunzo ya ufundi na teknolojia nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Aprili 10, 2026 kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Hussein Mohamed, amesema mafanikio hayo yanadhihirisha utekelezaji wa maono ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha elimu yenye ujuzi, ubunifu na tija kwa maendeleo ya uchumi wa taifa.
Amesema Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko la ajira na viwanda.
“Mheshimiwa Rais amekuwa akisisitiza kuwa hatuhitaji elimu ya vyeti pekee, bali elimu yenye ujuzi, ubunifu na tija. Kupitia uwekezaji huu mkubwa, vijana wetu wataweza kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa taifa,” amesema.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mafanikio ya DIT yanaonesha umuhimu wa kuunganisha elimu na sekta ya viwanda ili wahitimu waweze kuwa sehemu ya uzalishaji na maendeleo ya uchumi unaotegemea sayansi na teknolojia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Tanzania Bureau of Standards (TBS), Ashura Katunzi, amesema utoaji wa cheti hicho unaonesha kuwa taasisi hiyo imekidhi viwango vya kimataifa katika utoaji wa huduma za elimu.
Amesema DIT imekuwa taasisi ya kwanza nchini kupata cheti hicho cha ISO 21001:2018, hatua inayothibitisha kuwa mfumo wake wa usimamizi wa elimu unazingatia ubora unaotambulika kimataifa.
“Cheti hiki ni ushahidi wa kazi kubwa, nidhamu na dira ya maendeleo ya taasisi. Kinaonesha kuwa wanafunzi wanaopata elimu hapa wanapewa maarifa yanayowaandaa kwa ajira na ushindani katika soko la dunia,” amesema Katunzi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi hiyo, Masika, amesema hatua ya kupata cheti hicho ni matokeo ya safari ndefu ya maboresho ya mifumo ya uendeshaji iliyoanza mwaka wa fedha 2021/22, kwa lengo la kuhakikisha ubora wa elimu unatambulika kimataifa.
Ameeleza kuwa cheti hicho kinahusu kampasi zote tatu za taasisi hiyo ambazo ni Dar es Salaam, Mwanza na Songwe, na kwamba utekelezaji wake utaimarisha zaidi ubora wa mafunzo, kuongeza uaminifu kwa wanafunzi na wadau, pamoja na kuongeza ushindani wa wahitimu katika soko la ajira.
Masika amesema mafanikio hayo pia yanachangia utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2023 na malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya taifa kuelekea Tanzania Development Vision 2050, hasa katika kuimarisha rasilimali watu wenye ujuzi.
Amesisitiza kuwa taasisi hiyo itaendelea kuimarisha mifumo ya ubora, kufanya tathmini za mara kwa mara na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha elimu ya ufundi na teknolojia nchini inaendelea kukidhi viwango vya kimataifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...