Nchi 26 Duniani kesho Aprili 5,2026 zinatarajia kuingia katika kinyang'anyiro cha mashindano ya kusoma quran yanayotarajiwa kufanyika Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.



Kufuatia mashindano hayo leo April 4,2026 Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakari Zuberi na jopo la kamati ya maandalizi wamepokea ugeni mkubwa kutoka Saudi Arabia kumpokea Imamu Mkuu wa Msikiti Mtakatifu wa Makka, Imamu Badri Al Turki.

Akizungumza na vyombo vya habari Imamu Mkuu wa Msikiti wa Makka Badri amesema amefurahi kufika nchi ya Tanzania inaonesha jinsi nchi za Afrika hasa Tanzania inavyopenda amani na kuendeleza Maendeleo ya dini kwa ujumla.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Maimamu Tanzania(JUMADA) Imamu Suleiman Abdallah ametoa wito kwa Waislamu kote nchini kutumia fursa hiyo adhimu kumpokea mgeni huyo kuhudhuria katika mashindano hayo ikiwa na pamoja na kupata maombi ya imamu mkubwa duniani.

"Tukiwa kama Maimamu tumefurahi sana ujio Imamu Mkuu wa msikiti wa Makka sisi tutaitumia kama fursa" amesema Suleiman



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...