MPAMBANO mwingine wa kibabe umefika Jumatano hii katika dimba la Civitas Metropolitano kati ya Atletico Madrid dhidi ya Arsenal ambao ni vinara wa ligi kuu ya Uingereza.

Atletico Madrid na Arsenal hii ni moja za mechi ya kutazama katika mashindano ya UEFA Champions League inatarajiwa kuwa mechi ya kuvuta hisia za mashabiki wengi Duniani huku kila timu ikipewa nafasi ya kushinda mechi hii.

Kwa upande wa Atletico Madrid, timu hii inajulikana kwa mfumo wake wa kiulinzi uliokamilika chini ya mbinu za Diego Simeone. Atletico ni timu inayopenda kujenga msingi wake kwenye nidhamu, umakini na uwezo wa kuvumilia presha kubwa kutoka kwa wapinzani.

Hawapendi kucheza soka la kumiliki mpira muda mrefu, bali wanapendelea kusubiri nafasi na kushambulia kwa kasi pale mpinzani anapokuwa amezubaa. Wachezaji kama Antoine Griezmann, Koke, Solorth, Alvarez na wengine ni muhimu sana kwenye safu ya ushambuliaji siku ya leo.

Ukiachana mechi hiyo ya UEFA, Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Arsenal kutoka kule Uingereza, chini ya Mikel Arteta wamejijengea sifa ya kucheza soka la kisasa linalotegemea umiliki wa mpira, kasi ya maamuzi na mzunguko wa pasi wa haraka na safu bora ya kuzuia huku wakiwa wameruhusu mabao machache kwenye michuano hii.

Martin Odegaard ndiye injini ya ubunifu katikati ya uwanja, akitoa pasi za mwisho na kuongoza tempo ya mchezo. Upande wa mashambulizi, Bukayo Saka ni tishio la mara kwa mara kutokana na kasi yake, dribbling na uwezo wa kufunga mabao katika nafasi ndogo.

Takwimu zinaonesha kuwa mara ya mwisho kukutana timu hizi mbili, vijana wa Simeone walipoteza vibaya sana. Lakini sasa wanakutana kwenye Nusu Fainali moja ya mechi ambayo ni muhimu sana kwa wote wawili kwani kila timu haijawahi kushinda taji hili.

The Gunners mpaka sasa kutoka kwenye makombe 4 ambayo alikuwa anayawania, amebakiza mawili pekee huku nayo inabidi aongezee bidii ili aweze kuchukua. Kule EPL mpaka sasa licha ya kuwa anaongoza ligi bado presha ni kubwa kwani anayeshika nafasi ya pili ambayo ni City ana mchezo mmoja mkononi.

Huku kwenye UEFA ndio kadri michuano inavyozidi kusogea mbele, ndivyo ambavyo mechi zinazidi kuwa ngumu, hivyo Arteta akifanya mzaha anaweza kujikuta amekosa makombe yote tena na msimu huu.

Atletico yeye baada ya kukosa Kombe la Copa del Rey, sasa nguvu zote zimehamia kwenye UEFA ambapo sasa inabidi washinde mechi hii dhidi ya Arsenal huku nafasi ya kwenda hatua ya Fainali akipewa mwenyeji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...