NA VICTOR MASANGU, DAR

Maelfu ya wananchi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, taasisi na mashirika binafsi ,mashabiki wa soka na mziki wa dansi pamoja na wananchi mbali mbali .... wamejitokeza kwa wingi katika makaburi ya Kinonddoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara maarufu na mshabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Simba Emmanuel Nderimo almaarufu Macha ambaye alifariki dunia machi 30 mwaka huu.

Katika mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM),yaligubikwa na vilio na majonzi makubwa ambayo yalipelekea baadhi ya watu kushindwa kujizuia kwa kutokwa na machozi wakati wa kuuaga mwili huo.

Moja kati ya viongozi maarufu ambao walihudhuria msiba huo ni Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba Murtaza Mangungu akiwa ameambtana na viongozi wengine mbali mbali wa klabu hiyo, ambapo amesema marehemu Emmanuel alikuwa na mchango mkubwa sana katika klabu hiyo kwani alikuwa mstari wa mbela katika kusaidia mambo mbali mbali

Pia Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro naye alikuwa ni mmoja wa viongozi wa ulinzi na usalama ambaye naye alifika kwa ajili ya kutoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Emmaanuel Nderimo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe,Silvestry Koka ambaye marehemu ni shemeji yake hakusita kumwelezea marehemu jinsi alivyokuwa ni mpambanaji katika mambo mbali nmbali na kwamba alikuwa ni mtu wa kusamehe sana pindi unapomkosea na kwamba alikuwa ni mstari wa mbele katika kutoa ushauri wenye kujenga.

"Kwa kweli mimi nimesimama hapa kwannza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutukutanisha hapa katika msiba wa ndugu yetu Emmanuel lakini kitu ambacho nataka kukisema inapaswa tuishi kwa kupendana sana na ndio maana marehemu alikuwa na upendo mkubwa sana na watu mbali mbali na alikuwa ni mwepesi sana katika suala la kusamehe kwa hivyo inapaswa tujifunze mazuri ambayo ametuachia."amebainisha Mhe. Koka.

Nao baadhi ya viongozi na mashabiki akiwemo Mama Asha Baraka ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amesema kwamba ameguswa na kusikitishwa sana na msiba huo mzito kwani marehemu kwa upande wake alikuwa ni moja ya mtu muhimu sana katika kuleta chachu ya maendeleo katika ttimu pamoja na kuweza kusaidia mtu mmoja mmoja kwa hivyo ni pengo kubwa sana ambalo ameliacha.

Pia mwimbaji maarufu wa mziki wa dansi hapa nchini Ally Choki ni moja kati ya wasanii maarufu ambao walihudhulia katika msiba huo hadi kuweza kufika katika makaburi hayo ya Kinondoni kwa lengo la kumpumzisha ndugu yao na rafiki mkubwa wa burudani ya mziki wa dansi hapa nchini katika bendi mbali mbali.

Mazishi hayo ya marehemu Emmanule Nderimo ambayo yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam yameweza kuhudhuliwa na umati wa maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa chama, viongozi wa madhehebu ya dini, taaasisi wezeshi,wasanii maarufu, pamoja na wananchi ambao wamewza kufika na kumuhifadhi katika nyumba yake ya milele.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...