Na MWANDISHI WETU
MWENGE wa Uhuru umeridhia miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 13.3 iliyotekelezwa wilayani Kisarawe, mkoani Pwani na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza katika mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Wazo Mwang’onda, ame miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii.
Akiweka jiwe la Msingi katika mradi wa Barabara ya Maswi ,Pugu Kazimzumbwi yenye urefui wa kilometa 0.55 ambayo ujenzi wake ymagharimu sh. milioni 650, Mwang’onda alipongeza uongozi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kuzingatia viwango vilivyo elekezwa na thamani ya fedha.
“Mwenge wa Uhuru umekagua na kupitia taarifa za ujenzi wa barabara hii. Barabara imekidhi vigezo hivyo Mwenge wa Uhuru umeridhia kuzindua babara hii,”amesema Mwang’onda.
Barabara hiyo iliyopo kitongoji cha Bomani ipo chini ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA).
Aidha Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi na kufungua Mradi wa wa kitengo cha huduma za kibingwa za macho katika Hospitali ya Wilaya Kisarawe.
Mwang’onda, amepongeza hatua ya Wilaya ya Kisarawe kutoa huduma za kibingwa za machona kueleza dhamira ya Rais Dk. Samia ni kusogeza huduma bora za afya kwa wananchi.
Pia Mwenge wa Uhuru 2026 umezindua mradi wa kikundi cha vijana walionufaika na mkopo wa sh. milioni 35 za Halmashauri Wilaya ya Kisarawe.
“Rais Dk. Samia, ameelekeza vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wakopeshwe fedha hizi. Vijana hawa wamekopa fedha na wameanzisha shughuli hii ya uselemala. Mwenge wa Uhuru umefurahishwa na hatua hii,”amesema.
Ametoa wito kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu kuunda vikundi na kutumia fursa hiyo ya kukopa fedha halmashauri kujiinua kiuchumi.
Mradi mwingine uliomulikwa na Mwenge wa Uhuru ni Kiwanda cha Saruji cha Lucky Cement ambapo Mwang’onda alisema uwekezaji huo ni matunda ya utunzaji wa amani iliyopo nchini.
“Bila amani taifa haliwezi kuwa na uwekezaji mkubwa kama huu. Tuendelee kulinda amani ili kuvuta wawekezaji wengine kama hawa,”amesema.
Pia Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Mradi wa Maji wa Msanga kwenda vijiji vya Bembeleza na Chole.
Mradi huo uliogharimu sh. milioni 441 unatekelezwa na Wakala wa Majisafi Vijijini (RUWASA) na unatarajia kuondoa kero ya uhaba wa maji katika vijiji hivyo ukihusisha ujenzi wa tanki linalo chukua lita 90,000.
“Mwenge wa Uhuru umefurahishwa na utekelezaji wa mradi huu muhimu wa maji. Dhamira ya Rais Dk. Samia ni kuhakikisha maji safiyanapatikana hasa katika maeneo ya vijijini. Wito wangu wananchi wautunze mradi huu ili uwanufaishe,”amesema Mwang’onda.
Aidha Mwenge wa Uhuru umekagua mradi wa matumizi ya nishati safi na kupokea taarifa ya klabu ya mapambano ya rushwa katika Sekondari Menoromango katika Kijiji cha Menoromango, Kitongoji cha Kazimzumbwi.
Pia ulizindua mradi wa ujenzi wa madarasa mawili yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari Kisarawe.
Awali akiwasilisha taarifa mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, alisema ulipitia, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya jumla y ash.bilioni 13.3.
Magoti, amesema Kisarawe inapiga hatua kubwa ya maendeleo hivyo kumshukuru Rais Dk. Samia kwa kuelekeza fedha nyingi za miradi zilizo gusa kila sekta, hususam elimu, afya, miundombinu ya barabara, maji, uwezeshaji wananchi kiuchumi na utalii.





.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...