Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, leo Aprili 17, 2026 ameipokea Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyofanya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na taasisi mbalimbali za sekta ya afya Tanzania Bara.
Ziara hiyo imehusisha kutembelea Makao Makuu ya Wizara ya Afya, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Bohari ya Dawa (MSD).
Akiongea mara baada yakuwapokea, Dkt. Samizi amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya kwa lengo la kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Amesema kuwa juhudi hizo zimejikita kuimarisha miundombinu ya afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kuboresha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nasra Nassor, amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa wajumbe wa kamati kwani imewapa fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa sekta ya afya.
Ameongeza kuwa maarifa waliyoyapata yatawasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya Zanzibar kwa kuzingatia mifumo na mbinu walizojifunza kutoka Tanzania Bara.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...