Kampuni ya Sanlam Allianz Life Insurance (Tanzania) Limited imezindua rasmi Salama Plan, mpango mpya wa mafao unaolenga kuwasaidia Watanzania wanaokaribia au waliokwisha kustaafu kupata kipato cha uhakika kwa maisha yao yote, pamoja na usalama wa kifedha wa muda mrefu.
Uzinduzi wa mpango huo, umefanyika katika hafla maalum jijini Dar es salaam na kujikita katika kujibu hitaji kubwa na linaoongezeka kwa wastaafu wengi la kuwa na kipato cha uhakika na cha muda mrefu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa Sanlam Allianz Tanzania, Julius Magabe, alisema:
“Uzeeni unapaswa kuwa muda wa kupumzika, si wa kuwa na wasiwasi. Kupitia ‘Salama Plan’, tunawawezesha watu kufurahia matunda ya kazi zao kwa kujiamini, bila hofu ya kutokuwa na uhakika wa fedha.”
Mpango wa Salama ni suluhisho la kifedha ambalo linakuwezesha mtumiaji kuweka fedha mara moja (one-time premium) nakuweza kupokea pesa yako kila wakati. Wateja wanaweza kuchagua ratiba ya malipo kulingana na mahitaji yao. Kiasi cha chini cha kujiunga na huduma hiyo ni shilingi milioni 5 za Kitanzania, bila kuwa na ukomo wa kiwango cha fedha cha juu, hivyo kufanya bidhaa hii kuwafikia watu wengi zaidi, hususani wale wanaojiandaa kustaafu au waliokwisha kustaafu.
Mbali na kuleta suluhisho la kipato kwa maisha yote ya mstaafu, mpango huu pia unazingatia ustawi wa familia pale mteja anapofariki, kwa kuhakikisha kuwa wanufaika walioteuliwa wanaendelea kupokea malipo kwa kipindi kilichochaguliwa. Aidha, mpango huu pia unatoa nafasi ya dhamana (gurantee periods), vinavyolinda mapato ya mtumiaji wake hata baada ya kifo cha mteja ndani ya muda huo.
Bidhaa hii inalenga zaidi watu wenye umri kati ya miaka 50 hadi 70, wakiwemo wastaafu kutoka sekta ya umma na binafsi, wajasiriamali waliolenga kupunguza shughuli zao za kiuchumi, pamoja na watu wasiokuwa na mifumo rasmi ya pensheni lakini waliokusanya akiba au mali kwa muda.
Akisisitiza umuhimu wa bidhaa hiyo, Magabe aliongeza:
“Tunaelewa changamoto zinazowakabili wastaafu wengi, ikiwemo jukumu la kusaidia familia pana na kupanda kwa gharama za maisha. ‘Salama Plan’ ni namna yetu ya kuwaambia mmefanya wajibu wenu, sasa ni wakati wa kufurahia hatua inayofuata ya maisha.”
Uzinduzi wa bidhaa hii unaashiria mwelekeo mpya kwa Watanzania katika kujiandaa na maisha baada ya ajira, huku ukitoa uhakika wa kwamba urithi wao utaendelea kulinda familia zao. Hafla hiyo pia ilihusisha mijadala ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa pensheni, viongozi wa jamii na washauri wa kifedha, jambo lililoimarisha nafasi ya Sanlam Allianz kama mshirika anayeaminika katika mipango ya kustaafu nchini.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...