Dar es Salaam, Tanzania 

Tunatambua ongezeko kubwa la hivi karibuni la bei za mafuta ambalo limeongezeka kwa asilimia 33. Kama jukwaa linalolenga kusawazisha unafuu wa nauli kwa abiria na mapato endelevu kwa madereva, tunaendelea kushirikiana na mamlaka husika pamoja na wadau wengine kutathmini athari kamili za mabadiliko haya.

Miongoni mwa hatua zinazoweza kuchukuliwa kufuatia mashauriano haya ni;i) kufanya marekebisho ya nauli kulingana na ongezeko la gharama za mafuta; na/auii) kutekeleza mikakati mbadala itakayo punguza athari zinazotarajiwa katika mapato ya madereva.

Tunapenda kuwahakikishia madereva wote kuwa ustawi wao ni kipaumbele kikuu cha jukwaa letu. 

Tunathamini utulivu wao na ushirikiano unaoendelea na abiria wakati tunachukua hatua za haraka kuelekea suluhu zitakazolinda mapato yao na kuhakikisha huduma zinaendelea kutolewa bila usumbufu kwenye jukwaa letu.

Tunaendelea kusisitiza dhamira yetu ya uwazi, usalama na uthabiti wa muda mrefu katika mfumo wa usafiri nchini Tanzania.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...