Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Njombe,Kamati ya Michezo ya Meimosi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeshiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika  katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Njombe.

Katika zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka awewahimiza Wafanyakazi na wananchi kuhakikisha kuwa wanapanda miti yenye kuleta faida hususan miti ya matunda ili kusaidia upatikanaji wa kipato cha mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.

" Kumekuwa na tabia ya watu wengi kupanda miti kwaajili ya kivuli tu, pasipo faida yoyote, vi vizuri sasa tukapanda miti yenye kuleta faida kubwa kama vile miti ya matunda, amesema Mtaka.

Zoezi hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe, Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Mwenyekiti wa Kamati ya Meimosi na Watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...