Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeweka rekodi mpya kwa kukusanya shilingi trilioni 3.58 katika mwezi wa Machi 2026 pekee, ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 107.6 ya lengo lililowekwa.

Mafanikio hayo yameiwezesha TRA kukamilisha robo ya tatu ya mwaka wa fedha (Januari hadi Machi 2026) kwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 9.31, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.6 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Ufanisi huo umetokana na maboresho makubwa ya mifumo ya TEHAMA, hususan kuanza kutumika kwa mfumo mpya jumuishi wa kodi za ndani (IDRAS) mwezi Februari 2026, uliowezesha kusajili walipakodi wapya zaidi ya 69,000 pamoja na kuunganishwa kwa taasisi 92.

Aidha, kuimarika kwa mfumo wa forodha wa TANCIS kumechangia kuharakisha uondoshaji wa mizigo na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato katika vituo vyote vya forodha nchini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mafanikio hayo yanatokana na utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhimiza ulipaji kodi wa hiari kupitia ujenzi wa mahusiano mazuri kati ya TRA na walipakodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...