Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KATIKA Kuendelea kuboresha huduma kwa watanzania Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) kupitia faida ya Shilingi Bilioni 22.98 iliyotengeneza kwa mwaka wa fedha 2024/2025 limenunua na kukabidhi idara ya ufundi magari saba aina ya Hilux yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.6 pamoja na bajaji 28 zenye thamani ya shilingi  milioni 291.2 na kuzielekeza idara na vitengo kutumia vitendea kazi hivyo kwa kuwafikia na kutoa huduma kwa wakati kwa wateja na kufikia malengo ya kuwaunganisha na huduma wateja milioni moja kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi magari na bajaji hizo kwa wakuu wa Idara na Vitengo vya Shirika hilo Mkurugenzi mkuu wa TTCL Moremi Marwa amesema, vitendea kazi hivyo vimelenga kuwafikia kwa wakati wateja wanaotumia huduma kutoka Shirika hilo ikiwemo watumiaji wa huduma ya Faiba Mlangoni kwako.

`` Magari pamoja na bajaji hizi zitatumiwa na mafundi na watumishi wanaohudumia wateja, pindi huduma zinapokatika au wateja kupata hitilafu katika utumiaji wa huduma mafundi wetu watawafikia kwa wakati na kutatua changamoto na kwa ufanisi zaidi. “Amefafanua.”

Aidha amesema; Shirika hilo pia limenunua magari matano aina ya Hiace ambayo yatapokelewa mwisho wa mwezi huu mahususi kwa ajili ya masoko na mauzo kwa kuwafikia wateja wao pamoja na kuwafikia wateja wapya na kufafanua kuwa vifaa hivyo ni sehemu ya faida iliyotengenezwa na Shirika hilo ili kuweza kuhudumia wateja wao kwa ufanisi zaidi na kupata mapato yatakayoendeleza Shirika na kutoa gawio kwa Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufundi wa TTCL Mhandisi. Cecil Francis amemshukuru Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo kwa kusimamia maamuzi hayo ya kimkakati kwa kuhakikisha kunakuwa na vitendea kazi vitakavyorahisisha utoaji huduma na kuwafikia wateja wengi zaidi na kuwataka wafanyakazi wa Shirika hususani Idara ya ufundi kuvitumia vitendea kazi hivyo kwa madhumuni yaliyowekwa ili kuleta tija kwa Shirika na watumiaji wa huduma za TTCL.

Cecil ameeleza kuwa wamejidhatiti katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati pamoja na kuhakikisha wanafikia mikoa yote nchini na kuhakikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya mawasiliano na kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia inatimia.

Mkurugenzi wa Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Moremi Marwa akizungumza wakati akikabidhi magari na bajaji hizo kwa Idara na Vitengo na kuwasisitiza kutumia vitendea kazi hivyo kwa malengo na kuleta matokeo chanya katika utoaji huduma. Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Moremi Marwa (kulia,) akikabidhi mfano wa funguo kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika hilo Vedastus Mwita (kushoto,) Leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Moremi Marwa (kulia,) akikabidhi mfano wa funguo kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika hilo Mhandisi. Cecil Francis (kushoto,) Leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...