Na.Vero Ignatus, Arusha

Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na michezo imeendesha mafunzo kwa waandaa maudhui mtandaoni Mkoani Arusha yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo ili kuleta tija kwa kazi zao katika majukwaa mbalimbali ya mitandaoni

Akizungumza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na sanaa CPA Nyakaho Mturi Mahemba Mafunzo amesema mafunzo hayo yalikuwepo na watoa mada mbalimbali kutoka kwa wabobevu ambapo mada hizo zitawasaidia kuzalisha maudhui mazuri yenye maadili katika jamii yanayothamini utu na nchango wa Mtanzania katika shughuli za kila siku.

Aidha amesema lengo la mfuko huo wa Utamaduni nia thabiti ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwapatia fursa vijana waaoandaa maudhui mtandaoni kwa kuwapatia mikopo wenye riba nafuu Kukuza, kuendeleza na kuimarisha sekta ya sanaa na utamaduni kwa manufaa ya kijamii na kiuchumi.

"Mfuko huu unalenga Kukuza ajira kupitia sanaa kwa vijana na wadau wa sekta Kuinua ubora wa kazi za sanaa ili ziweze kushindana ndani na nje ya nchi uchochea uchumi wa ubunifu una lengo la kusaidia sera za serikali katika kukuza sekta ya sanaa"

Mahemba amesema Vile vile katika mafunzo hayo wametoa Elimu ya fedha namna ya kuweka Akiba elimu ya urasimishaji, na uwekezaji ambapo itawasaidia waandaa maudhui kukopo kwa nidhamu nakusimamia mitaki yao vyema ili iweze kuwa na tija.

Mafunzo hayo yaneweza kushirikisha waandaa maudhui mtandaoni zaidi ya 450 ambapo waikuwepo na watoa mada mbalimbali wabobevu.

Baada ya kuwezeshwa mtaji tumieni vizuri katika maeneo mliyokusudia na mrudishe kwa wakati ili wengine nao waweze kunufaika rudisheni mikopo kwa wakati hiyo ili wengine nao wanufaike.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Kelvin Kanje amesema mafunzo hayo ya awamu ya kwanza kwa watengeneza Maudhui mtandaoni yalianzia mkoa wa Dar es salama, Mwanza ambapo wamehitimisha mkoani wa Arusha .

Aidha amesema mafunzo hayo ni ahadi aliyoutoa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia. Suluhu Hassan kwa kutangaza fursa kwa vijana kwa kutoa Bil 50 ambapo wengine wameshakopa n kuchukua fedha huku wengine wakiendelea kujipanga .

Kwa upande wake mtengeneza Maudhui Mtandaoni Fahad Fuad amesema wakati sahihi wa kutengeneza maudhui ameeleza kwa kina mbinu na mikakati ya kuchagua muda wenye tija ili kufikia hadhira kwa ufanisi zaidi.

Amefafanua umuhimu wa kuelewa tabia za watazamaji, sambamba na majukwaa yanayotumika pamoja na mzunguko wa matumizi ya mitandao ili kuongeza ushawishi na mwonekano wa maudhui

Aidha Mafunzo haya ya awamu ya kwanza jijini Arusha yanawaleta pamoja wabunifu wa maudhui ili kujifunza, kubadilishana uzoefu, na kuboresha ubora wa kazi zao. Hii ni hatua muhimu katika kukuza uchumi wa kidijitali na kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya maudhui ya mtandaoni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na sanaa  CPA Nyakaho Mturi Mahemba
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Kelvin Kanje akizungumza na waaandaaji mudhui mtandaoni Jijini Arusha





Washiriki wa mafunzo na waaandaaji maudhui mtandaoni

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...