Na  Diana Byera, Bukoba 

WIZARA ya Katiba na Sheria imeanza kutoa mafunzo kwa wajumbe wa bodi za usuluhishi wa migogoro ya ndoa, kutokana na ongezeko la kesi za talaka nchini, 

Akifungua mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria  Franklin Rwezimula  amesema mafunzo hayo yameanzia mkoani Kagera kwa  lengo la kuongeza weledi na mbinu mpya za  usuluhishi wa ndoa katika jamii ili kujenga familia bora na jamii yenye mshikamano 

“Takwimu zinaonyesha talaka zilizosajiliwa mwaka 2023 zilikuwa  711,  mwaka 2024  zikapanda hadi 1,569, na  mwaka 2025 talaka  zilizosajiliwa zilikuwa 1,172 na hizo ni zile talaka tu zilitoleawa taarifa na ndoa nyingine zimekuwa zikivunjika kimya kimya  bila kutolewa taaarifa na kuhatarisha   ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.”

Amefafanua bodi za usuluhishi zinapaswa kufanya kazi kwa weledi na kujiepusha kuwa mahakimu huku akidai bodi hizo zisiwe sehemu ya kupokea rushwa  Bali zijikite kuondomitafaruku  kutovujisha Siri na Kutenda haki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa umma  Obadia Kamea  amesema uwepo wa wajumbe wa bodi ya usuluhishi Kwa ngazi ya kata nchi nzima unalenga kupunguza Mrundikano wa  kesi za talaka zinazoenda mahakamani  

Amesema pia mafunzo haya yanalenga kuimarisha mbinu mpya , usuluhishi kulingana na hali ya kisasa ya malalamiko  makubwa ya ndoa na migogoro  iliyopo kwa sasa ukilinganisha na miaka ya Zamani .

Awali Issaya Tendega ambaye ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera amesema migogoro ya ndoa isipotatuliwa kwa wa wakati inasababisha ofisi za viongozi ngazi ya wilaya na mikoa  kuwa na mrundikano wa kesi ambo ambalo linasababisha viongozi kutumia muda mrefu Kufanya usuluhishi kuliko kufanya kazi Nyingine.

"Ofisi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wanapokea kesi nyingi za ndoa na zinatumia muda mrefu sana ,tunaamini wajumbe wa haya mabaraza wakifanya kazi yao vizuri migogoro ya ndoa itapungua ,tunaomba baada ya mafunzo haya mfaye kazi kwa weledi ili kupunguza kesi nyingi za ndoa mahakamani na ofisi za viongozi"alisema Tendega

Awali Jawadu Mwanandege ambaye ni Mjumbe wa bodi  ya usuhishi wa ndoa ameishukuru Serikali kwa namna inavyoendela kuimarisha mafunzo na mbinu za utatuzi kwa ngazi ya mabaraza ambapo alisema kuwa Mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya usuluhishi na kufanya kazi kwa haki.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...