WIZARA ya Kilimo imesema mafanikio katika kilimo cha mpunga nchini yametokana na uwekezaji wa kimkakati wa Serikali, huku ikiielekeza COPRA kuimarisha usimamizi wa masoko ili kuongeza tija.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Zao la Mpunga uliofanyika Machi 30, 2026 mkoani Morogoro, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayesimamia Maendeleo ya Mazao na Usalama wa Chakula, Prof. Peter L. M. Msofe, alisema sekta hiyo imepata mageuzi makubwa.
Alisema uzalishaji wa mchele umefikia tani milioni 2.6 katika mwaka 2024/2025, ukilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 1.2, hali iliyoifanya Tanzania kuwa na ziada ya tani milioni 1.4.
Prof. Msofe aliongeza kuwa ziada hiyo imewezesha kuuza nje tani 298,715 za mchele katika masoko ya EAC na SADC na kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 333.5 za fedha za kigeni.
Pamoja na mafanikio hayo, alibainisha kuwa bado kuna fursa ya kuongeza tija zaidi, akieleza kuwa wastani wa uzalishaji ni tani 3.2 kwa hekta dhidi ya uwezo wa kufikia tani 6 kwa hekta.
Aidha, alisema Serikali inalenga kuongeza uzalishaji hadi tani milioni 8 ifikapo 2030 na kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno kutoka asilimia 25 hadi chini ya asilimia 10.
Kwa upande wa COPRA, Bi. Pendo Biganmbo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mazao na Viwango, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, alisema wameanza usajili na utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wa mpunga ili kuimarisha usimamizi wa soko.
Alisema zoezi hilo litahusisha pia wakulima kusajiliwa pamoja na mashamba yao ili kuongeza ufanisi katika mnyororo mzima wa thamani wa zao la mpunga.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...