Na Mwandishi Wetu 

IMEELEZWA kuwa Maji ya kimataifa ni moja ya rasilimali inayoleta amani katika nchi mbalimbali zinazonufaika na wananchi wake.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifungua kikao cha 13 cha  Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (ZAMCOM) jijini Dar es salaam amesema maji hayana mpaka na yanakusanya watu kwa maendeleo yao.

Aweso ambaye katika mkutano huo ni Mwenyekiti ameainisha kuwa umoja wa wananchi na nchi walizopo umeletwa na maji ya kimataifa, maji yanayovuka mipaka ya nchi zao.

Amesema ni muhimu kuwa na rasilimali za kutosha ili kuleta maendeleo na wananchi wanashirikishwa kutunza rasilimali za maji ili kuleta maendeleo katika sekta nyingine za uchumi.

Waziri Aweso amesisitiza kwa wajumbe wa mkutano huo kuwa maji ni muhimu na yanahitajika kuleta maendeleo kwa wananchi.

ZAMCOM inagusa maisha ya kila wananchi zaidi ya milioni 51 na imekusanya nchi za Tanzania, Angola, Zambia, Malawi, Namibia, Botswana, Zimbabwe, na Msumbiji.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...