Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Ushirika nchini (Coop-Bank), Godfrey Ng’urah, amesema benki hiyo imejipanga kuhakikisha wakulima wanalipwa asilimia 50 ya fedha zao kabla ya mnada kufanyika na asilimia 50 iliyobaki kulipwa baada ya mnada, hatua inayolenga kuongeza uwazi na kuharakisha malipo kwa wakulima.

Mura aliyasema hayo mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala yaliyofanyika Mei 19 jijini Dodoma. 

Alieleza kuwa mkakati huo utasaidia kuondoa changamoto ya ucheleweshaji wa malipo ambayo imekuwa ikiwakwamisha wakulima katika shughuli zao za uzalishaji.

Aidha, alisema Coop-Bank itaendelea kushirikiana kwa karibu na vyama vya ushirika na wadau wa sekta ya kilimo ili kuwawezesha wakulima kupata huduma za kifedha kwa wakati, jambo litakaloongeza tija katika uzalishaji na kuimarisha uchumi wa wakulima pamoja na maendeleo ya sekta ya kilimo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...