Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Godfrey Eliakimu Mnzava, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, viongozi wa siasa, pamoja na timu ya wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, amefanya ziara ya kikazi kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopendekezwa kupitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mnzava alikagua mradi wa Kituo cha Mafuta cha Mavoa kilichopo Kitongoji cha Njiapanda Magharibi, Kata ya Njiapanda, pamoja na mradi wa Zahanati ya Ghona uliopo Kijiji cha Ghona katika Kata ya Kahe Mashariki.
Aidha, Mkuu wa Wilaya na timu yake walifika katika Shule ya Sekondari Mwika ambapo ndipo litakapokuwa eneo la mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, eneo ambalo pia Mwenge utajionea programu maalum ya matumizi ya Nishati Safi.
Miradi mingine iliyofanyiwa ukaguzi ni pamoja na ujenzi wa barabara katika Kata ya Kilema Kusini, mradi wa maji wa Kijiji cha Mabungo uliopo Kata ya Kirua Vunjo Kusini, pamoja na mradi wa vijana na uzalishaji wa madini ya ujenzi.
Vilevile, ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kimochi na ujenzi wa Shule ya Amali ya Sekondari Chemchem iliyoko Manushi katika Kata ya Kibosho Magharibi.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2026 zinatarajiwa kuingia mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Juni 2026 na kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ifikapo tarehe 01 Julai 2026.
Mwenge huo utaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo.
.jpeg)







.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...