KAMPUNI ya ubashiri ya Meridianbet imeendelea kuonyesha kuwa mafanikio yana maana zaidi pale yanapogusa maisha ya watu. Kupitia programu zake za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kampuni hiyo imetoa msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto cha UMRA Children Center kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umejumuisha mahitaji muhimu kama mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari pamoja na bidhaa nyingine zinazotumika kila siku na watoto hao. Hatua hiyo imekuja kama sehemu ya kuendelea kusaidia makundi yenye uhitaji maalum ndani ya jamii.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram alisema kampuni hiyo inaamini kuwa jamii ndiyo nguvu kubwa ya maendeleo, hivyo ni muhimu kusaidiana na kushikana mkono pale inapowezekana.

“Watoto wanahitaji mazingira bora, malezi na upendo ili waweze kutimiza ndoto zao. Sisi kama Meridianbet tunaona fahari kuwa sehemu ya furaha yao kupitia msaada huu,” alisema mwakilishi huyo.

Uongozi wa UMRA Children Center umeipongeza Meridianbet kwa moyo huo wa kujitolea huku ukieleza kuwa msaada huo utasaidia kupunguza changamoto za mahitaji ya kila siku na kuleta tabasamu kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...