MAAFISA Habari wa Serikali wametakiwa kuongeza ufanisi katika kutangaza shughuli za Serikali huku wakizingatia mabadiliko ya teknolojia.

Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe,  Anthony Mtaka wakati akifunga Kikao Kazi cha 21 cha Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki, na Uhusiano Serikalini leo Mei10, 2026.

Mtaka amewaeleza maafisa hao kuendelea kuwa daraja kati ya Serikali na wananchi kwa kuwapatia taaarifa sahihi zinazolenga kubadilisha maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu pamoja na fursa zilizopo katika sekta ya burudani.

"Mnapohudhuria vikao kazi hivi tafuteni pia fursa ambazo zitabadilisha maisha yenu binafsi nje ya kazi, tafuteni uwekezaji katika biashara, kilimo na sehemu nyingine ili kuwa na maisha bora zaidi baada ya kustaafu", ameseisitiza Mtaka.

Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari -MAELEZO  aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kelvin Kanje akimkaribisha Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa, Kikao Kazi hicho kimekuwa na mafanikio kwa kuwa maafisa wamepata elimu na mafunzo mbalimbali  yanayolenga kuongeza ufanisi katika majukumu yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Eleuteri Mangi, amesema kikao kazi hicho kimekuwa chachu ya maafisa kujipima utendaji kazi wao na chachu ya kufanya vizuri katika taasisi zao, akisisitiza vikao hivyo kuendelea kufanyika.

Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,  Pettu Ogilo amesema kikao kazi hicho kimekuwa na manufaa kwake kwani masuala mengi wanayoelekezwa yanamsaidia katika utekekezaji wa majukumu yake, pia amepata elimu pamoja na kubadilishana uzoefu na maafisa wenzie. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...