Na MWANDISHI WETU
Taasisi ya Saratani Ocean Road, imeanza kutoa huduma bora za kisasa kwa kutumia mtambo wa tiba mionzi ya nyuklia kwa wagonjwa wa saratani.
Daktari Bingwa wa Tiba Mionzi ya Nyuklia wa taasisi hiyo, Tausi Maftaha, amesema wameanza kutoa matibabu kwa kutumia mtambo huo wa kisasa ambao una uwezo wa kuelekeza tiba na kutengeneza dawa za saratani.
Amesema mtambo huo una uwezo wa kutengeneza dawa, ambazo awali walikuwa waagiza kutoka Ulaya na Afrika Kusini.
"Tulikuwa tunaagiza dawa kutoka katika nchi zilizoendelea pamoja na Afrika Kusini, lakini kutokana aina hizi za dawa haziishi muda mrefu yaani huwezi kuweka kama za kawaida maabara au Famasi, hizi ni dawa ambazo unatengeneza katika mtambo, ikishatengenezwa inatakiwa mgonjwa atumie hapo hapo", amesema.
Dk. Tausi amesema serikali kwa kuona hilo, ikaamua kufanya uwekazaji mkubwa wa kuwa na mtambo huo na taasisi ndiyo itakuwa kituo kikuu cha kusambaza dawa hizo katika hospitali nyingine na nchi jirani.
Amesema dawa zinazotengeneza zinachunguza aina zote za saratani ispokuwa saratani ya damu ambayo mfumo wake tofauti.
Aidha Dk. Tausi amesema dawa hizo zinafaida nyingi zikiwemo mgonjwa kupewa dawa sahihi, inafupisha muda wa matibabu, inaokoa gharama kwa wagonjwa kwasababu dawa za saratani gharama zake ziko juu.
Pia amesema mitambo hiyo ya kisasa ndiyo inayotumika kutoa matibabu ya saratani katika nchi ziliendelea na umefungwa na kampuni ya kimataifa.
"Ni utaalamu wa kisasa ukienda, Ulaya, India, Afrika Kusini utaikuta mitambo hii, kwahiyo huduma tunayotoa hapa ndiyo hiyo hiyo inayitolewa nchi za nje, hivyo hakuna sababu ya mgonjwa kwenda kupata huduma hiyo nje ya nchi, labda kama mahitaji binafsi", amesema.
Dk. Tausi amemshukuru Rais Dk. Samia kwasababu aliaanza na mradi huu tangu akiwa Makamu wa Rais na ametoa fedha hadi sasa umekamilika, ameokoa fedha nyingi.
Aidha Dk. Tausi amewataka wananchi kutokuwa na hofu ya kuwa mionzi nyukilia ina madhara, alisema mionzi hiyo ni tiba na kwamba wananchi wawe na utaratibu wa kufika mapema katika hospitali kupata huduma kabla matatizo hayajawa makubwa.
Amesema waondokane na dhana potofu kwamba mwenye saratani akifanyiwa upasuaji huwa wanapoteza maisha, upasuaji moja ya tiba kuhakikisa mgonjwa anapona.
Dk. Tausi amesema mgonjwa wa saratani akiwahi kupata matibabu mapema anapona kabisa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...