Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Ruvuma limezindua ofisi ndogo ya TANESCO katika kijiji cha Nyerere, kata ya Mtina wilayani Tunduru, kwa lengo la kusogeza huduma za umeme karibu na wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amemwagiza Meneja wa TANESCO pamoja na timu yake kuhakikisha wanaitumia ofisi hiyo kufanya kazi usiku na mchana ili kutatua changamoto za umeme katika kata ya Mtina na maeneo ya jirani.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma, Boniface Malibe, amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kusogeza huduma zote muhimu karibu na wananchi wa kata hiyo, ambao hapo awali walilazimika kufuata huduma mjini umbali wa zaidi ya kilometa 40.

Amesema uwepo wa ofisi hiyo utasaidia kupunguza ucheleweshaji wa kushughulikia hitilafu mbalimbali za umeme na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi.

Nao wananchi wa kata ya Mtina wameeleza kuwa eneo hilo limekuwa likikumbwa na changamoto za umeme kwa muda mrefu, lakini wameonesha matumaini makubwa kufuatia uzinduzi wa ofisi hiyo ndogo ya TANESCO, wakiamini itarahisisha upatikanaji wa huduma na utatuzi wa changamoto zinazojitokeza.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...