Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Mei 14, 2026 amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Andrew Lentz na kufanya majadiliano kuhusu Mkataba Mpya wa Ushirikiano (MoU) wa Afya kati ya Marekani na Tanzania
Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Ofisi ya Waziri wa Afya, ulisisitiza dhamira ya pamoja ya nchi zote mbili katika kuimarisha usalama wa afya, huku ukilenga kuboresha mashirikiano katika maeneo mbalimbali ya Sekta ya Afya ikiwemo huduma za tiba, mafunzo kwa wataalamu pamoja na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini
Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Mchengerwa amefafanua kuwa Serikali itaendelea kuthamini ushirikiano mzuri ulioimarika kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Marekani kwenye huduma za afya.
Amesema kupitia mashirikiano hayo, Tanzania imeendelea kunufaika katika maeneo mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya magonjwa ya mlipuko, huduma za mama na mtoto pamoja na ujenzi wa uwezo kwa wataalam wa afya.
Aidha, ujumbe wa Ubalozi wa Marekani umeeleza utayari wao wa kuendelea kushirikiana na Serikal a Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya afya yenye lengo la kuboresha huduma kw: wananchi.
Kikao hicho pia kilijadili namna ya kuongeza ushirikiano katika matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye sekta ya afya, ukuaji wa ujenzi wa viwanda na vifaa tiba, tafiti za kitabibu pamoja na kubadilishana uzoefu kati ya wataalamu wa afya wa Tanzania na Marekani.
Katika majadiliano hayo upande wa Serikali ya Tanzania uliongozwa na Mheshimiwa Mchengerwa, Katibu Mkuu, Daktari Seif Shekalaghe, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Dawa na Vifaa Tiba Emmanuel Tayari, Mganga Mkuu wa Scrikali, Daktari Grace Magembe na Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara, Rahibu Mashombo, huku Ujumbe Wa Ubalozi ukiongozwa na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Andrew Lentz na Maafisa waandamizi wa Ubalozi huo





.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...