Kampuni ya Climb Up Limited imeeleza kuwa matumizi ya mizani janja ya kidigitali yanaweza kuwa suluhisho muhimu katika kuondoa changamoto za udanganyifu wa vipimo zinazowakabili wakulima, wafugaji na wafanyabiashara nchini.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Emmanuel Ngallah, amesema teknolojia hiyo imeundwa kwa mfumo wenye ulinzi wa hali ya juu unaosaidia kuhakikisha vipimo haviwezi kuchezewa wala kufanyiwa udanganyifu.
Katika maadhimisho hayo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, alitembelea banda la Climb Up Limited kwa kushirikiana na WMA na kupata fursa ya kujionea namna mizani hiyo ya kidigitali inavyofanya kazi pamoja na mchango wake katika kuongeza uwazi na usahihi wa vipimo kwenye shughuli za biashara na kilimo.
Ngallah amesema kuwa kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo imeendelea kuleta maboresho ya kidigitali yatakayosaidia kuongeza ufanisi na kuimarisha imani kwa watumiaji wa mifumo ya vipimo nchini.
Aidha, kampuni hiyo imebainisha kuwa matumizi ya mifumo ya kidigitali kupitia stakabadhi za ghala yamerahisisha uhifadhi wa taarifa za wakulima na usimamizi wa mazao yanayohifadhiwa maghalani, jambo linalochangia kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo na biashara.




.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...