Wanajumuiya wa Shirika la INADES Formation Tanzania wamelitaka shirika hilo kubuni miradi ya kilimo itakayosaidia kuwavutia vijana kuingia katika sekta hiyo, wakiamini inaweza kuwa njia ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Patrick Lameck wakati wa Washa iliyofanyika kuelekea mkutano mkuu wa mwaka wa wanajumuiya na wadau wa shirika hilo, unaoenda sambamba na uchaguzi wa viongozi.

Lameck amesema ili kupanua wigo wa utendaji wa shirika hilo, ni muhimu kuanzishwa kwa miradi ya kilimo itakayowapa vijana fursa ya kushiriki shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato.

Amesema bado vijana wengi wanaogopa kujihusisha na kilimo kutokana na dhana iliyozoeleka kuwa sekta hiyo haina faida, hali inayochangia kupungua kwa ushiriki wao.

“Tunaomba viongozi wetu wabuni miradi ya kilimo, kwa sababu itasaidia kushawishi vijana kujiunga na shughuli hizo na kuboresha maisha yao.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa INADES Formation Tanzania, Jacqueline Nicodemus, amesema wanajumuiya wanapaswa kuwa na mshikamano na ushirikiano ili kuwezesha shirika hilo kufikia malengo na mikakati iliyojiwekea.

Amesema mafanikio ya shirika yatategemea ushiriki wa pamoja wa wanachama katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazopangwa.

“Tunapaswa kuwa kitu kimoja na kushirikiana katika utekelezaji wa mipango yetu ili kuhakikisha shirika linaendelea kupiga hatua.”







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...