Zaidi ya wafugaji 200 wa Kanda ya Ziwa wamepata elimu kuhusu matumizi ya mifumo ya kidigitali katika sekta ya mifugo, iliyotolewa na kampuni ya climb Up Limited, ili kuwawezesha wafugaji kuongeza tija katika uzalishaji wa mifugo bora na kuachana na mbinu za ufugaji ambazo zimepitwa na wakati.
Hayo yameelezwa na Afisa Masoko wa kampuni hiyo, Jackline Cosmas, Mei 31 mkoani Shinyanga wakati wa kuhitimisha Maonyesho ya Mifugo ya Kanda ya Ziwa yaliyofanyika kwa muda wa siku mbili.
Baadhi ya wafugaji waliotembelea banda la Climb Up Limited na kupata mafunzo hayo wamesema elimu waliyoipata itawasaidia kubadilisha mtazamo wao kuhusu ufugaji, kutoka katika mbinu za jadi na kuelekea ufugaji wa kisasa unaotumia teknolojia kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na ufanisi.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...