Airtel Tanzania imezindua minara miwili mipya ya mawasiliano ya 4G inayotumia umeme wa gridi ya taifa katika mikoa ya Geita na Dodoma, hatua inayotarajiwa kuboresha upatikanaji wa simu na intaneti kwa maelfu ya wananchi wa maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekosa mawasiliano ya uhakika.

Minara hiyo imejengwa katika Kata ya Nyaruyeye, Wilaya ya Geita, na Kijiji cha Chinagali, Kata ya Zoissa, Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, ikiwa na lengo la kuboresha mawasiliano, huduma za intaneti na huduma za kifedha kupitia simu kwa jamii zilizokuwa zikikabiliwa na changamoto za mtandao kwa miaka mingi.

Tofauti na minara mingine ya vijijini inayotegemea majenereta, minara hiyo imeunganishwa na umeme wa gridi ya taifa huku ikiwa na majenereta ya akiba, hatua inayopunguza gharama za uendeshaji na kuchangia uhifadhi wa mazingira kupitia kupunguza matumizi ya mafuta.

Katika Kata ya Nyaruyeye, zaidi ya wananchi 15,000 pamoja na wakazi wa Kata ya Nyarugusu na maeneo jirani wanatarajiwa kunufaika na maboresho hayo.

Uwekezaji huo unafuatia tathmini iliyofanywa na Airtel baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo hayo.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha mawasiliano, kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kufungua fursa za kidijitali kwa jamii.

Viongozi wa maeneo husika wamesema minara hiyo itasaidia shughuli za elimu, biashara na utoaji wa huduma za umma, pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi, hususan katika maeneo yanayojishughulisha na kilimo na ufugaji kama Wilaya ya Kongwa.

Airtel imesema uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wake wa kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata fursa sawa katika uchumi wa kidijitali kupitia upatikanaji wa miundombinu ya mawasiliano ya uhakika



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...