Serikali ilitenga takribani shilingi bilioni 3 katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya na uboreshaji wa miondombinu katika Wilaya ya Mbogwe, Mkoa wa Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Edwin Bayona, ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.
Bayona ameeleza kuwa fedha hizo zimetumika kujenga shule mpya ya msingi, kuongeza mabweni kwa wanafunzi wa kike, pamoja na matundu ya vyoo.
Aidha, Mkoa wa Geita umepokea takribani walimu wapya 1000. Wilaya ya Mbogwe imepata walimu 115 wa shule za msingi na sekondari ili kuongeza kasi ya ufundishaji katika miradi inayoendelea.
Mkuu wa Mkoa, Martin Shigela, amesema ziara hiyo ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo huku akiwapongeza wananchi wanaoendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa miundombinu katika sekta ya elimu.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...