Na Nasra Ismail, Geita

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Karia Rajab Magaro, Juni 25, 2026 ametembelea mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa Nkome Kata ya Nkome, Wilaya ya Geita. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea maendeleo ya mradi unaotarajiwa kuchochea biashara na ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.

Akizungumza na mkandarasi wa mradi, kampuni ya RIN Contractor and General Supplies Company Ltd, Magaro amemuelekeza kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi ukamilike na kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa Julai 2026 kama ilivyoelezwa kwenye mkataba.

Amesema Serikali inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili wananchi wapate miundombinu bora inayokidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.

Mradi huo unafadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita - GGML kwa gharama ya Shilingi 473,909,792.82 hadi kukamilika. Ujenzi wa soko hilo unatarajiwa kuimarisha biashara, kuongeza ajira na kuinua kipato cha wananchi wa Nkome na maeneo jirani.

Akitoa taarifa ya maendeleo, Mhandisi wa mradi Eng. Edson Missana amesema soko hilo la kisasa litakuwa na uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara na watumiaji zaidi ya 80 kwa wakati mmoja. Pia lina jengo la vyoo matundu 10 pamoja na mabafu maalumu kwa matumizi ya wafanyabiashara na wananchi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...