Na.Ashura Mohamed - Arusha

Katika kuhakikisha kuwa Uchumi wa wakazi wa mkoa wa Arusha unaimarika wananchi wa mkoa huo hususani Vijana wametakiwa kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa mbali mbali za kiuchumi ili kunufaika na ujio wa mashindano ya kimataifa ya Afcon 2027.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini bw.Jospeh Mkude,wakati wa Kongamano la Vijana la Engutoto Youth Summit kuhusu Mashindano ya AFCON 2027,Wakili Irene Ndosi ambaye ni Katibu Tarafa Suye amesema kuwa ujio wa Afcon ni neema kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Arusha ambapo mbali na kupata burudani ya mpira wa miguu lakini pia ni fursa kwa makundi yote kuongeza uchumi wao.

"Fursa zitaanzia kuanzia watu wa chini kabisa boda boda,watu wa usafirishaji mpaka wanawake watengeneza shanga,kila mtu achukue nafasi hiyo kuleta mabadiliko chanya kwenye uchumi wake binafsi na familia yake na mkoa kwa ujumla,pia tuwe tayari kujaza eneo la uwanja wa Afcon kwasababu mashindano haya ni yakipekee na yanashirika nchi tatu ambazo ni Tanzania,Kenya na Uganda."Amesitiza Ndosi

Aidha Hamza Juma Njiku ni Diwani wa Kata ya Engutoto amesema kuwa kongamano hilo ni muhimu kwa kuwa limewakutananisha vijana na wadau mbal8 mbali katika kuonyesha fursa zilizopo kuelekea mashindano hayo ya Afcon.

"Sisi katika kata yetu fursa za Afcon zimetugusa moja kwa moja kwa kuwa tunajengewa Uwanja mkubwa mzuri wa Mazoezi kwaajili ya mashindano hayo ambapo utakuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 5000 waliokaa,maegesho ya magari 500 na mabasi mawili kwaajili ya zile timu ambazo zitaingia kufanya mazoezi,ila uwanja ukikamilika na mashindano kumalizika utatumika kwaajili ya ligi kuu na michuano mbali mbali."Amesema Diwani Njiku

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Kata ya Engutoto ambaye ndio muandaaji wa Kongamano Engutoto Youth Summit,bw.Ibzan Michael Ruheta amesema kuwa kongamano hili si jukwaa la kisiasa bali ni jukwaa linalokutanisha watu wote kujadili fursa za AFCON kuelekea mwaka 2027.

Bw.Ruheta amesema kuwa Mashindano ya AFCON hayatahuishwa na Tanzania peke yake bali ushirikiano na mataifa mengine wakiwemo Kenya pamoja na Uganda,hivyo kama Watanzania ni wajibu wao kuamka na kuhakikisha tunaitumia nafasi hiyo ipasavyo.

"Ndugu mgeni rasmi, kama unavyojua nchi yetu imepata fursa ya kuandaa mashindano haya ya AFCON,hivyo kama viongozi mliopo katika nafasi za maamuzi, ni vizuri kujipanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na taasisi mbalimbali zilizopo nchi yetu kwa kikisha fursa hizi tunazipata kwa wakati, vijana waheshimiwe, wasikilizwe na kero zao zitatuliwe ili nchi yetu inufaike."Amefafanua Mwenyekiti huyo

Kongamano la Engutoto Youth Summit lenye kauli mbiu ya "Unlocking 2027 AFCON Opportunity" limeandaliwa na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Engutoto,na limekusudia kuwajengea vijana uwezo wa kunufaika na fursa za michezo hiyo kubwa ya kimataifa ambapo limefanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) na kukutanisha Vijana Zaidi ya 1000 ili kuonesha nyanja mbali mbali ambazo vijana wanaweza kunuifa nazo.
Picha ya Viongozi Mbali Mbali wa Chama na Serikali walioshiriki Kutoa Mada  katika Kongamano la Engutoto Youth Summit kupelekea Mashindano ya AFCON 2027.
Mgeni rasmi Wakili Irene Ndossi ambaye ni katibu Tarafa ya Suye akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini akizungumza na Vijana ambao hawapo pichani
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Engutoto mwenye Tisheti Nyeupe Bw.Ibzan Ruheta akiwa katika picha ya Pamoja na Wadau Mbali mbali
Safu ya Viongozi wa Chuo kutoka Chuo Cha Arusha Technical(ATC) ikiongizwa na Raisi wa Serikali ya wanafunzi  Bw.Magolosa Mosses mwenye  Suti nyeusi Kulia,mara baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo katika Chuo Cha Uhasibu Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...