Na Janeth Raphael MichuziTv Bungeni - Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu, Khadija Shaban Taya, amesema kuwa anawaheshimu wanaume kwa nafasi yao katika jamii kama baba na kaka, lakini ameeleza kuwa sehemu kubwa ya changamoto za mmomonyoko wa maadili inatokana na baadhi ya wanaume kushindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yao ya kifamilia, hali inayosababisha wanawake kubeba mzigo mkubwa wa uangalizi wa familia.
Akichangia hoja hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalum Kwa mwaka wa fedha 2026/27 amesema kuwa pale wanaume wanaposhindwa kusimama katika majukumu yao ya malezi na uongozi wa familia, wanawake hujikuta wakilazimika kutoka na kujitafutia kipato ili kuhakikisha watoto wanapata mahitaji ya msingi.
Amefafanua kuwa hali hiyo imekuwa na athari za kijamii, ikiwemo kuongezeka kwa changamoto za malezi na kuporomoka kwa misingi ya maadili katika baadhi ya familia.
“Kwa hakika hakuna mwanamke mwenye akili timamu anayependa kumuumiza mwanaume anayempenda na kumheshimu. Wanawake wengi wanajikuta wakibeba majukumu makubwa kwa sababu ya mazingira yaliyopo,” amesema.
Aidha, Mbunge huyo ameeleza kuwa kuna baadhi ya wanaume wanaotelekeza familia zao, ikiwemo watoto wenye ulemavu, hali inayosababisha wanawake kuachwa peke yao katika mzigo wa malezi na matunzo.
Ameongeza kuwa katika baadhi ya familia, watoto wenye ulemavu wamekuwa wakikosa msaada wa baba zao, jambo linalosababisha changamoto kubwa kwa akina mama wanaojitahidi kuwalea na kuwahudumia bila msaada wa karibu wa kifamilia, wakati mwingine hata kukumbana na kutengwa na baadhi ya ndugu na jamii.
Katika wito wake kwa Serikali, Khadija Shaban Taya ameiomba kuangalia kwa karibu kundi la watoto wenye ulemavu na wazazi wao, ili kuhakikisha wanajumuishwa kikamilifu katika sera na mipango ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na utekelezaji wa haki zao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...