Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BENKI ya NMB imezindua rasmi NMB Mkononi Super App ikiwa ni jukwaa jipya la kidijitali linalolenga kubadili namna Watanzania wanavyosimamia maisha yao ya kifedha kwa kuweka huduma mbalimbali za benki, uwekezaji, akiba, mikopo na bima katika mfumo mmoja wa kisasa.
Akizungumza leo Juni 16,2026 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema uzinduzi wa Super App hiyo unaashiria mwanzo wa enzi mpya ya huduma za kifedha nchini zinazokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa na cha baadaye.
"Kuzingatia mahitaji ya leo na ya kesho, tunapoizindua Super App tunazindua namna mpya ya Watanzania kusimamia maisha yao ya kifedha, namna mpya ya kulinda maisha yao kupitia bima, namna mpya ya kuwekeza na kuweka akiba," amesema.
Amesema dunia imebadilika kwa kasi ambapo huduma nyingi sasa zinapatikana kupitia simu za mkononi, hivyo ni muhimu sekta ya fedha nayo kwenda sambamba na mabadiliko hayo.
"Leo watu wanasoma kupitia simu, wanasafiri kupitia simu, wanawasiliana kupitia simu na hata maisha yao ya kila siku yako kwenye simu. Sasa tumekusanya huduma zote muhimu za kifedha sehemu moja kwa urahisi, usalama na kasi inayoendana na mahitaji ya mteja wa sasa," amesema.
Zaipuna amesema NMB imeboresha mfumo huo baada ya kusikiliza maoni ya wateja wake waliotaka huduma nyingi zaidi zipatikane kupitia programu moja.
Miongoni mwa maboresho hayo ni uwezo wa mteja kuona akaunti zake zote katika sehemu moja bila kulazimika kutumia mifumo tofauti, pamoja na uwezo wa kuziunganisha mwenyewe ndani ya programu.
Aidha, amesema wateja sasa wanaweza kuweka standing orders kupitia simu zao, jambo litakalowarahisishia kufanya uhamisho wa fedha au kuweka akiba kwa wakati bila kukumbushwa kila mwezi.
Kwa mujibu wa Zaipuna, Super App hiyo pia imeongeza uwezo wa kufungua akaunti mpya kidijitali bila kufika tawi lolote la benki.
"Mteja hatahitaji kufika benki wala tawi lolote. Ataweza kufungua akaunti yake mwenyewe kupitia simu yake popote alipo," alisema.
Aliongeza kuwa mfumo huo unamwezesha mteja kupata taarifa mbalimbali za kifedha, kufuatilia mwenendo wa matumizi na kufanya maamuzi bora ya kifedha kupitia taarifa zinazopatikana ndani ya programu.
Zaipuna alisema hata watu ambao si wateja wa NMB sasa wanaweza kupakua programu hiyo na kuanza safari ya kujiunga na huduma za benki kwa urahisi.
Kuhusu huduma za mikopo, alisema kupitia Super App mteja binafsi anaweza kuomba mkopo wa hadi shilingi milioni mbili moja kwa moja kupitia simu yake, huku wafanyabiashara wadogo na wa kati wakipata fursa ya kuomba mikopo ya hadi shilingi milioni tano.
Amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa teknolojia uliofanywa na benki hiyo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ili kuhakikisha huduma zake zinakidhi viwango vya kimataifa.
Katika kuelezea umuhimu wa programu hiyo kwa vijana, Zaipuna alisema kizazi cha sasa kinahitaji huduma zinazopatikana muda wote na zinazokwenda sambamba na kasi ya maisha ya kidijitali.
"Vijana wa leo wanataka kusimamia fedha zao kupitia simu. Simu imekuwa biashara, benki na sehemu ya maisha yao ya kila siku. Hii Super App imejengwa kwa ajili yao na kwa ajili ya Watanzania wote," amesema.
Amewahimiza pia wabunifu wa teknolojia na wajasiriamali wa kidijitali kutumia fursa iliyopo ndani ya mfumo huo kuendeleza ubunifu wao kwa kushirikiana na NMB.
Kwa mujibu wake, benki hiyo inayohudumia zaidi ya wateja milioni 10 inalenga kuifanya Super App kuwa jukwaa la huduma mbalimbali za kifedha na biashara.
Zaipuna amesema moja ya huduma muhimu zilizoboreshwa ni usimamizi wa vikundi vya kijamii na kiuchumi kupitia mfumo huo.
Amesema vikundi vitaweza kufungua akaunti, kuwaalika wanachama, kuweka kanuni zao za uendeshaji, kusimamia michango, mikopo ya ndani na kutoa taarifa za kifedha kwa uwazi zaidi bila kulazimika kukutana ana kwa ana.
"Vikundi vimekuwa shule ya kwanza ya elimu ya fedha kwa Watanzania wengi. Kupitia mfumo huu vitapata uwazi, usalama na ufanisi zaidi katika usimamizi wa fedha zao," amesema.
Ameeleza kuwa wanachama wataweza kuona michango yao, taarifa za kifedha na kushiriki maamuzi muhimu popote walipo kupitia simu zao.
Katika hatua nyingine, amesema Super App hiyo imeanza pia kutoa huduma za ununuzi wa bima kidijitali, ikiwemo bima za magari, pikipiki na mali dhidi ya moto.
Kwa mujibu wake, mteja anaweza kujinunulia bima au kumnunulia mtu mwingine kwa kutumia taarifa za msingi kama namba ya usajili wa gari au taarifa nyingine zinazohitajika, hatua inayorahisisha upatikanaji wa huduma za bima nchini.
Amesisitiza uzinduzi wa NMB Mkononi Super App ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuendelea kuongoza mapinduzi ya huduma za kifedha kidijitali nchini kwa kuwapatia Watanzania huduma salama, rahisi na zenye kasi zinazowawezesha kufikia malengo yao ya kifedha.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...